Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imetangaza bei mpya za umeme ambazo zimepanda kwa kuzingatia makundi tofauti ambayo ni..

Mkurugenzi wa Uchumi Mdhibiti wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za
Nishati na Maji (Ewura), Felix Ngamlagosi akizungumza na waandishi wa
habari Dar es Salaam jana, alipokuwa akitangaza viwango vipya vya bei ya
umeme. Kulia ni Mkurugenzi wa Umeme wa mamlaka hiyo, Anastas Mbawala.
Picha na Silvan Kiwale
---
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura)
imetangaza bei mpya za umeme ambazo zimepanda kwa kuzingatia makundi
tofauti.
Akizungumza na waandishi wa habari jana,
Mkurugenzi Mdhibiti Uchumi wa Ewura, Felix Ngamlagosi alisema bei mpya
zitaanza kutumika Januari Mosi, 2014 mpaka Desemba 2016. Hata hivyo,
alisema mabadiliko ya bei yanaweza kutokea katikati ya kipindi hicho cha
miaka mitatu.
Bei mpya ya umeme
Bei mpya ya umeme
Ngamlagosi alisema mwananchi wa kipato cha chini
anayetumia uniti (0-75) kwa mwezi, atalazimika kulipia Sh100 kwa uniti
ukilinganisha na Sh60 iliyokuwapo awali.
Ongezeko lipo pia katika kundi linaoitwa T1 la
watumiaji wakubwa wa umeme wa nyumbani, ambao watalipia Sh306 kwa uniti
ikiwa ni ongezeko la Sh85 ya bei iliyopo sasa.
Alisema katika kundi la T2 la wateja wakubwa
wanaopimwa kwenye matumizi ya uniti 7,500, malipo ya uniti moja
yamefikia Sh205 ikiwa ni ongezeko la Sh73 kutoka bei ya sasa.
“Kundi jingine la T3-MV ambao ni wateja wa viwanda
vikubwa, litaanza kulipia Sh166 kwa uniti ikiwa ni ongezeko la Sh45 ya
bei ya sasa pamoja na kundi la T3HV lililounganishwa kuanzia voti 66,000
na zaidi ambalo litaanza kulipia Sh159 kwa uniti ikiwa ni ongezeko la
Sh53,” alisema Ngamlagosi.
No comments:
Post a Comment