Header Ads

FRANSCISCO KIBASA NA MAGHAMA JUMMADAS WAIBUKA WASHINDI WA SHINDANO LA UANDISHI NA INSHA NA UCHORAJI


SONY DSC
Meneja Uhusiano wa Multchoice, Barbara Kambogi akiongea na waandshi wa habari pamoja na wadau mbalimbali wakati wa hafla hiyo.
HABARI PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE DAR ES SALAAM
……………………………………………………………………..
FRANSCISCO Kibasa na Maghma Jammadas wameibuka washindi wa shindano la kuwasaka wanafunzi wakali wa uandishi a isha na uchoraji nchini linaloendeshwa na Kampuni ya MultiChoice kila mwaka.
Meneja Uhusiano na kampuni hiyo, Barbara Kambogi aliwatangaza rasmi washindi katika hafla maalum ya wanahabari iliyofanyika jijini Dar es Salaam Disemba 12-2013.
“Kwa kutambua umuhimu wa elimu, MultiChoice imeamua kuwa bega kwa bega na Serikali kuhakikisha Watanzania wengi wananufaika na mfumo mpya wa elimu ambao ni wa kisayansi zaidi. Shule wanazotoka wanafunzi hawa tumezipatia pia zawadi maalum ya dishi na kisimbuzi ambacho kina channel maalum nane za elimu,” alisema Barbara.
Kibasa, mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mzunzumbe, Morogoro, aliibuka mshindi wa insha nzuri ya masuala ya satelaiti akifuatwa na Fabian Shayo kutoka shule hiyo pia. Kwa ushindi huo, Kibasa na wazazi wake watapata ofa ya kwenda Afrika Kusini mwakani kuangalia namna matangazo ya satelaiti yanavyorushwa.
Kwa upande wake, Maghma aliyeshinda uchoraji wa picha nzuri za satelaiti akifuatwa na Sanjma Joshi (wote kutoka Shule ya Sekondari Agha Khan Mzizima, Dar es Salaam), atasafiri na wazazi wake kwenda nchibni Ufaransa kuangalia namna roketi inavyorushwa angani.
Hafla hiyo iliyohudhuriwa na waharirir ma waandishi wa habari za michezo na burudani nchini, ilinogeshwa na wachezadansi wa Kundi la THT.

No comments:

Powered by Blogger.