EDIBILY JONAS LUNYAMILA ANAPUMUA KWA MSAADA WA MASHINE, NI BAADA YA KULAZWA HOSPITALI YA MWANANYAMALA AKISUMBULIWA NA KIFUA JIJINI DAR ES SALAAM.
Lunyamila akiwa amelala kitandani hospitalini jana.PICHA|MAKTABA
WINGA wa zamani wa Yanga na Taifa
Stars, Edibily Lunyamila, amelazwa katika Hospitali ya Mwananyamala na
anapumua kwa msaada wa mashine.
Mwanaspoti jana Jumatatu mchana
lilimshuhudia Lunyamila akiwa amelala katika kitanda namba 18 cha wodi
ya wanaume katika hospitali hiyo ya mkoa wa kitabibu wa Kinondoni.
Edibily Lunyamila akichanja mbuga.
Edibily Lunyamila akichanja mbuga.
Kwa mujibu wa Daktari, Madirisha
Pascal, aliyempokea na kumpatia huduma ya kwanza winga huyo wa zamani,
Lunyamila anasumbuliwa na tatizo la kifua ambalo linamfanya ashindwe
kupumua vizuri.
“Sasa anapumua kwa msaada wa mashine
na bado tunaendelea kumfanyia uchunguzi ili kubaini nini kinachomsumbua
zaidi,” alisema Pascal.
Ndugu wa Lunyamila aliyemfikisha
hospitali hapo aitwaye Lameck John, aliliambia Mwanaspoti kwamba
Lunyamila alianza kujisikia vibaya juzi Jumapili na jana Jumatatu
asubuhi hali yake ilibadilika ndipo alipomwahisha hospitali.


Winga hatari wa zamani klabu ya Dar es
salaam Young Africans Edibily Jonas Lunyamila, akimtoka beki wa zamani
wa Simba Mathias Mulumba, katika mchezo wa fainali ya kombe la Hedex
kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza katika miaka ya tisini, na
hii ilikuwa ni muda mfupi baada ya Lunyamila kutua nchini toka nchini
Ujerumani alikokuwa amekwenda kufanya majaribio ya kucheza soka la
kulipwa, na siku hii akiwapiga Simba moja kati ya mabao mawili na
lingine likifungwa na Bakari Malima kufuatia kona ya Lunyamila.
“Alikuwa analalamika hawezi kupumua na
kifua kinamsumbua pia mbavu zilikuwa zikimuuma, baada ya majibu ya
vipimo tutajua kinachomsumbua zaidi,” alisema Lameck.
Lunyamila hakuweza kuzungumza na mwandishi wa habari hii kwani alikuwa amelala.
Lunyamila aliyeichezea Yanga kwa
mafanikio katika miaka ya 1990, amewahi kuisaidia Yanga kucheza hatua
ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka
1998.http://www.mwanaspoti.co.tz
No comments:
Post a Comment