Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa:Tuliohuzunika, tutashinda pamoja

Waziri mkuu wa zamani na mbunge wa Monduli,Edward Lowassa,akiwapa
pongezi akina mama wa kikundi cha Msanja wilayani Monduli,baada ya
kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa wodi za wazazi katika hospitali ya
wilaya ya Monduli. PICHA|MUSSA JUMA
--
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amesema waliofurahi na kuhuzunika naye pia watashinda pamoja naye.
Bila kufafanua kauli yake jana, Lowassa aliwaambia
wakazi wa Monduli mkoani Arusha kuwa: “Kumbukeni kaulimbiu yangu wakati
wa Uchaguzi Mkuu uliopita, tulifurahi pamoja, tulihuzunika pamoja na
tutashinda pamoja”.
Mbunge huyo wa Monduli alikuwa akizungumza kwenye
mkutano wa hadhara mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa wodi
mbili za ghorofa za wazazi katika Hospitali ya Wilaya ya Monduli.
Katika hotuba yake fupi, pia alitamba kwamba
atayashinda majaribu. Hata hivyo, hakufafanua majaribu hayo... “Kuna
vita kubwa, lakini ambacho naweza kusema ni kuwa nayaweza yote kwa yeye
anitiaye nguvu.”
Kuhusu afya yake ambayo mara kadhaa imeelezwa kuwa
siyo imara, kiongozi huyo alisema kwa sasa ni nzuri na imeimarika
kupita kipindi kingine chochote.Kwa habari zaidi Bofya na Endelea.......
No comments:
Post a Comment