Header Ads

Ushauri Kutoka Kwa Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA(Mstaafu) Ananilea Nkya Kwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini-Chadema Zitto Kabwe na Dr Kitila, Mwigamba


Aliyekua  Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA Ananilea Nkya
----
Dr Kitila,  Mwigamba na mwanangu Zitto, 
Niwape ushauri kidogo.

Kama kweli haya tuliyoelezwa mmehusika, ni vema mkakubali kwamba kuna mahala mmepotoka kiasi. Sisi tunatambua kuwa binadamu huweza kukosea ili mradi mtu asifanye makosa kwa kukusudia.    Adhabu iliyotolewa  kwenu kuvuliwa vyeo, nionavyo mimi  utaratibu wa kibinadamu wa kurekebishana.Kama kweli mnahusika  kwa chembe katika haya, na kama kweli hamjanunuliwa kuvuruga  nia njema ya kujenga  upinzani imara wa kisiasa nchini kwa lengo la kuharakisha maendeleo ya wananchi na nchi kwa ujumla,  basi msiwe na papara. 
Tulieni tafakarini na kisha ombeni radhi. Ninaamini mkifanya hivyo, uongozi wa chama chenu,wanachama na Watanzania watawasamehe na kisha rudini kazini jengeni chama chenu kiweze kuimarika  zaidi kwa ajili ya  kuwatumikia Watanzania kwa umakini, uaminifu na ujasiri usiotiliwa shaka. 
 
Mkifanya hivyo mtajenga utaduni mpya wa kuigwa  nchini  na wanasiasana heshima yenu itapanda juu. Mkifanya vinginevyo, mnaweza  mkaonekana mliingia CHADEMA  kwa lengo la kuvuruga  au kutafuta umaarufu, fedha  au vyeo haraka haraka. 
Mungu awabariki.

No comments:

Powered by Blogger.