SERIKALI IMEDHAMIRIA KUFUTA UMASKINI KWA KUSAMBAZA UMEME VIJIJINI
Waziri
wa Nishati na madini Mh Sospeter Muhongo akisaini kitabu cha wageni
katika ofisi za CCM Mkoa wa Morogoro alipotembelea wakati akianza ziara
yake katika Mkoa wa morogoro.
Katika
ziara hiyo waziri Muhongo amesema Serikali ya CCM Imeamua Kutokomeza
kabisa Umaskini na ndiyo maana inasambaza Nishati ya Umeme kwa kasi
kubwa ili Nishati hiyo iwasaidie watanzania katika shuguli za uchumi
ikiwemo Elimu,Viwanda na matumizi Mengine.Aidha Waziri Muhongo Amesema
kuwa Kumekuwa na uharibufu Mkubwa wa Mazingira hali inayoashiria Jangwa
kutokana na uvunaji wa miti kwajili ya Uzalishaji wa Mkaa na wameamua
kusambaza Nishati ya Umeme kwa haraka ili kuiokoa nchi kuwa
Jangwa.Waziri muongo ameongeza kwamba kwa sasa Bei ya kuwaunganishia
wananchi umeme Imeshushwa Mpaka Shilingi 177,000/= tu kwa lengo la
kuwawezesha watanzania wenye pato la chini kuunganisha umeme na
kunufaika na Nishati hiyo.Pia waziri Muhongo ameongeza Shirika la Umeme
wameagizwa kupokea Fedha kidogo kidogo kwa wananchi wote watakohitaji
kuunganishiwa umeme na hawana Uwezo wa Kulipa fedha zote kwa Pamoja..
Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro Mh Joel Bendera Kushoto Akiwa na Mwenyekiti wa CCM
Mkoa wa morogoro ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mh
Innocent Kalogeris wakati walipompokea waziri wa Nishati na madini Mh
Sospert Muhongo Mjini Morogoro
Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa morogoro ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Morogoro
Kusini Mh Innocent Kalogeris Kushoto akiwa na Waziri wa Nishati na
madini Mh Sospeter Muhongo kulia wakisikiliza taarifa ya Chama cha
Mapinduzi Mkoa wa Morogoro Iliyokuwa inasomwa na Katibu wa ccm Mkoa wa
Morogoro hayupo pichani.
Waziri
wa Nishati na madini Mh Sospeter Muhongo Akiuliza jambo kwa Injinia wa
shirika la umeme mkoa wa morogoro Ndugu Maro walipotembelea Kituo cha
kuunganishia Umeme kilichopo Pangawe wakati wa ziara ya Waziri huyo ya
Kukagua miradi ya kusambaza Umeme vijijini Mkoani Morogoro
Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa morogoro ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Morogoro
Kusini Mh Innocent Kalogeris Akifafanua Jambo katika ziara ya waziri
huyo na kushoto ni Meneja Wa Tanesco Mkoa wa Morogoro Akisikiliza kwa
makini
Waziri
wa Nishati na madini Mh Sospeter Muhongo Akipokelewa na Viongozi katika
kata ya Mtamba Jimbo la Morogoro kusini lililopo Wilaya ya Morogoro
Vijijini alipotembelea Wilaya Hiyo wakati akikagua Mradi wa Kusambaza
Umeme vijijini Mradi Uliofadhiliwa na Shirika la Maendeleo La MCC.Waziri
Muhogo Amesema Serikali ina nia ya kusambaza Umeme Vijiji vyote
tanzania Ili kila mtanzannia afaidi nishati hiyo..
Waziri
wa Nishati na madini Mh Sospeter Muhongo Akisaini Kitabu cha wageni
kata ya Mtamba wilaya ya Morogoro Vijijini kabla ya kusikiliza kero za
Wananchi wa wilaya hiyo kuhusu Umeme na uchimbaji wa Madini
Wananchi wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Nishati na madini Mh Sospeter Muhongo
No comments:
Post a Comment