MIRADI YA MAJI MAKETE YALETA KIZAAZAA KWENYE KIKAO CHA DCC
Mradi wa maji uliopo Matamba.
=====
Kutokamilika kwa baadhi ya miradi ya maji na mingine kujengwa
chini ya kiwango kumeonekana kuwa mwiba mchungu kwa wananchi na baadhi
ya viongozi wapenda maendeleo wilayani Makete mkoani Njombe
Hayo yamebainika hii leo kwenye kikao cha kamati ya ushauri ya
wilaya (DCC) kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya
Makete wilayani hapo
Akizungumza kwenye kikao hicho, mwenyekiti wa halmashauri ya
wilaya ya Makete Mh. Daniel Okoka amesema kwa upande wa tarafa ya
Matamba amesema yeye kama mtia saini mikataba ya ujenzi wa miradi hiyo
hataipokea mpaka akatapofanya ukaguzi hatua kwa hatua
"Mimi nitakwenda Matamba na kuwafuata wananchi tunakwenda hatua
kwa hatua na kuzungumza nao wakati wa ukaguzi na wakiridhika na ujenzi
huo wa mradi, mimi nitaupokea wakikataa sitaupokea" alisema Okoka
Amesema kwa kiasi kikubwa anashangazwa na baadhi ya viongozi wa
Matamba ambao hakuwataja kumwambia kuwa hana mamlaka ya kufanya mikutano
kwenye maeneo hayo, na kufafanua kuwa yeye kama mwenyekiti wa
halmashauri ya wilaya ya Makete ana uwezo wa kufanya mikutano sehemu
yeyote ile ndani ya wilaya yake bila kizuizi, na hivyo viongozi hao
wasimkwamishe
Akichangia hoja hiyo, katibu wa CCM wilaya ya Makete Miraji
Mtaturu amesema ni aibu kwa viongozi pindi miradi ya maji inapoonekana
kutokamilika ilihali taarifa zinazotolewa zinaonesha kuwa miradi hiyo
imefanyika na imekamilika
Akizungumzia
mradi wa Matamba amesema hali ni mbaya kwani mradi huo hautoi maji
licha ya taarifa kudai kuwa umekamilika, na kudai kuwa huu si muda wa
kulumbana kumtafuta mchawi na badala yake kinachotakiwa ni maji
yawafikie wananchi na si kitu kingine
Naye
mwenyekiti wa kikao hicho ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Makete Josephine
Matiro ameagiza kuwa tatizo hilo la ukosefu wa maji katika maeneo
mbalimbali yenye changamoto ikiwemo Matamba lifanywe haraka iwezekanavyo
ukizingatia kuwa serikali imetoa kipaumbele kwa miradi hiyo ya maji
No comments:
Post a Comment