Header Ads

Mbunge wa Kinondoni, Iddi Azzan na kumlipa fidia ya gharama alizotumia katika shauri la madai ya kutotendewa haki na gazeti hilo, baada ya kuandika habari ambazo zilizomuhusisha mbunge huyo na biashara ya dawa za kulevya bila kumpa nafasi ya kujieleza.


Mbunge wa Kinondoni, Idd  Azzan  akieleza malalamiko yake mbele ya Kamati ya Maadili ya Baraza la Habari (MCT), kuhusiana na madai ya kukashifiwa na gazeti la Raia Mwema  na Mwanahabari kwa kumhusisha na biashara ya dawa za kulevya, jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mhariri wa Gazeti la Raia Mwema, Godfrey Dilunga. Picha na Joseph Zablon.  
---
 Gazeti la Raia Mwema limetakiwa kumwomba radhi ndani ya wiki mbili,Mbunge wa Kinondoni, Iddi Azzan na kumlipa fidia ya gharama alizotumia katika shauri la madai ya kutotendewa haki na gazeti hilo, baada ya kuandika habari ambazo zilizomuhusisha mbunge huyo na biashara ya dawa za kulevya bila kumpa nafasi ya kujieleza.

  Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Kamati ya Maadili ya Baraza la Habari (MCT),kilichofanyika makao makuu ya baraza hilo jana, Mwenyekiti wa MCT, Jaji Thomas Mihayo alisema, baada ya kamati hiyo kusikiliza pande zote mbili imebainika kuwapo kwa upungufu wa kitaaluma katika habari hiyo.
  Gazeti la Raia Mwema katika toleo namba 309 la Julai 31, mwaka huu kulikuwa na habari ambayo kichwa chake cha habari kilisomeka  ‘Idd Azzan Mbunge au muuza madawa ya kulevya’ na ndani ya habari hiyo kulikuwa na tuhuma kuwa anajihusisha na biashara ya dawa hizo huku baadhi ya vifungu vikimkariri mbunge huyo.Kwa habari zaidi Bofya na Endelea.........

No comments:

Powered by Blogger.