KINANA AWAUNGURUMIA WATENDAJI WA VYAMA VYA MSINGI USHIRIKA NA BAADHI YA WATENDAJI WA SERIKALI MKOANI RUVUMA.
Ndugu
Kinana na Ujumbe wakienda kukagua ujenzi wa jengo la Wodi ya Wazazi ya
akina mama na Watoto,kwenye hospitali ya Wilaya ya Namtumbo.
Pichani
kulia ni Mbunge wa jimbo la Namtumbo,Mh.Vita Kawawa,Katibu wa NEC,Siasa
Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye,Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana pamoja na
Katibu
wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt.ASharose Migiro wakishiriki
katika ujenzi wa msingi wa Wodi ya Wazazi na Watoto katika hospitali ya
Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.
Pichani
shoto ni Mbunge wa jimbo la Namtumbo,Mh Vita Kawawa pamoja na Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana wakishiriki kuchanganya sementi kwa ajili ya
ujenzi wa Wodi ya Wazazi ya akina mama na Watoto inayojengwa kwenye
hospitali ya Wilaya ya Namtumbo kwa ahadi ya Rais Jakaya Kikwete.
Jengoo la Utawala wa hospitali hiyo ya wilaya ya Namtumbo.
Pichani
shoto ni Mbunge wa jimbo la Namtumbo,Mh Vita Kawawa akimuongoza Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na ujumbe wake walipokuwa wakikagua majengo ya
hospitali hiyo.
Barabara ya kuelekea kwenye hospitali hiyo.
Katibu
Mkuu wa CCM akiwa ameongozana na Ujumbe wake wakipata taarifa ya mtambo
wa kufua umeme katika kituo cha kufua Umeme ndani ya Wialaya ya
Namtumbo.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akifungua shina la Wakereketwa la Waendesha
Bodaboda Wilayani namtumbo,Kinana aliwachangia vijana hao kiasi cha
shilingi milioni moja kwa ajili ya kuwafungulia akaunti ya benki,ili
waweze kupata mikopo ya kununua piki piki kwa ajili ya shughuli zao.
Katibu
wa NEC Siasa,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akiwahutubia wananchi wa wa
Lwinga kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Namtumbo kwenye
uwanja wa Taifa.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia
wananchi wa kijiji cha Lwinga kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika
mjini Namtumbo kwenye uwanja wa Taifa mkoani Ruvuma.Ndugu Kinana na
ujumbe wake wapo kwenye ziara ya kikazi mkoani Ruvuma,Mbeya na Njombe
katika kukagua Utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama cha
CCM,kusikiliza matatizo ya Wananchi ikiwa ni pamoja na kuwahimiza
kushiriki katika shughuli mbalimbali za kujiletea maendeleo. Katika
Ziara hiyo ya Tunduru na Namtumbo wananchi wamelalamikia kuhusu bei ya
zai la Korosho na Tumbaku,kama vile haitoshi wanancho hao walikwenda
mbali zaidi kwa kulalamikia suala zima la Mbolea.
Mbunge
wa Jimbo la Namtumbo Mh. Vita Kawawa akiwahutubia wananchi kwenye
mkutano wa hadhara mjini Namtumbo, mkutano huo umefanyika kwenye uwanja
wa Taifa.Vita Kawawa amewatuhumu baadhi ya viongozi wa vyama vya
ushirika na Ofisa Ushirika wa mkoa huo wa kuwambambikizia madeni
wakulima wa Tumbaku kupitia ruzuku ya mbolea,ambapo makadirio ya mbolea
inayohitajika kwa wakulima huongezwa kinyemela na Wananchi kuachiwa
mzigo mkubwa wa kulipa madeni ambayo hayawahusu,hali inayowapelekea
wakulima hao kutokuwa na imani na baadhi ya viongozi wa chama na
serikali.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza kwenye mkutano wa
hadhara na wananchi wa kata ya Mchomoro Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma
mara baada kupokelewa vyema na wananchi ya Wilaya hiyo ya Namtumbo.
Mbunge
wa jimbo la Namtumvo,Vita Kawawa akifafanua jambo kwa Katibu wa NEC
Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt.ASharose Migiro pamoja na Katibu wa
NEC Siasa,Itikadi na Uenezi,Nnape Nnauye ndani ya Kata ya Mchomoro
Wialayani Namtumbo mkoani Ruvuma.
Katibu
Mkuu wa CCM,ndugu Abdulrahman Kinana na ujumbe wake wakipata chai
nyumbani kwa balozi wa shina,Said Husein mara baada ya kuwasili katika
kijiji cha Mchomoro wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma.Kinana na ujumbe
wake kwenye ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya chama na kukagua
uhai wa chama katika mkoa wa Ruvuma
No comments:
Post a Comment