KINANA ASHIRIKI NA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO JIMBO LA RUNGWE MASHARIKI.
Ndugu
Kinana na Ujumbe wake wakipita kukagua jengo la Maabara katika shule
ya sekondari ya Mwakaleli,katika halmashauri ya Busokelo,Wilayani
Rungwe mkoani Mbeya.Mradi huo wa ujenzi wa madarasa na maabara ni
mpango serikali wa kuboresha shule za sekondari zilizopo kwenye kata
na Taifa kwa ujumla kwa kushirikiana na benki ya Dunia.
Pichani
chini, Ndugu Kinana akiwa amebeba tofali ikiwa ni sehemu ya ushiriki wa
ujenzi wa madarasa katika shule ya sekondari ya Mwakaleli,katika
Halmashauri ya Busokelo,wilayani Rungwe.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa nyumba za Walimu wa Shule ya Sekondari ya Mwakaleli.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha
Katende,katika halmashauri ya Busokelo wilayani Rungwe,mkoani
Mbeya,Kinana aliwaeleza kuwa CCM inatekeleza ilani yake ya uchaguzi na
kuongeza kuwa ahadi zilizoahidiwa zitatimizwa. Aidha Kinana alikazi pia
kuwa kama chama Imara lazima kihoji serikali juu ya pesa za ujenzi maendeleo ya wananchi,kwa nini hazitolewi kwa wakati. Ndugu
Kinana yupo mkoani Mbeya kwa zaiara ya siku 11 katika kutekeleza Ilani
ya CCM,kukagua miradi mbalimbali ikiwemo na kujua matatizo ama kero za
Wanachi.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kijiji cha
Katende ndani ya halmshauri ya Busokelo wilayani Rungwe mkoani
Mbeya,ambapo Nape aliwatahadharisha wakaji wa mji huo kuwa makini na
vyama vinavyojita vya siasa,kutokana na kuanza kupoteza dira na
muelekeo.
Katibu
wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akikata ubao
akiwa pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye,kwa ajili ya
ujenzi wa vyumba vya maabara na madarasa ya shule ya Sekondari ya
Mwakaleli.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye picha ya pamoja na
wazee wa kijiji ambao leo walimpa heshima ya kuwa Mzee wa Katende na
kumvisha mgolole kama heshima ya mtu mzima.
Katibu
wa NEC Siasa na Mahusiano ya Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akiwa
ameketi kwenye mkeka unaojulikana kama Kalili aliopewa zawadi na wakina
mama wa Katende,Wilayani Rungwe mkoani Mbeya.
Mzee
Issa Simion akitoa salaam kwa niaba ya wazee wa Kijiji cha Katende na
pia kushukuru kwa Serikali na Chama Cha mapinduzi na pia kuelezea kero
zinazohusu wakazi wa kata ya Katende.
Mbunge
wa Wanawake Mkoa wa Mbeya Dk.Mary Mwanjelwa akiwasalimia wakazi
Katende.katika halmashauri ya Busokelo,wilayani Rungwe mkoani Mbeya.
No comments:
Post a Comment