KAMATI KUU CHADEMA YAMTEUA TUNDU LISSU KUWA MWANASHERIA MKUU WA CHAMA
Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), imemteua
Mhe. Tundu Lissu kuwa Mwanasheria Mkuu wa chama hicho. Kamati hiyo
ilikaa kikao chake Novemba 20 mpaka 21 katika Hoteli ya Blue Pearl
Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam. Kamati Kuu pia imemteua Wakili Msomi Mh. Peter Kibatara kuwa Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu wa Chama hicho.
No comments:
Post a Comment