Hawa ndio mabilionea wanne vinara Tanzania Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Jarida la Marekani la Forbes
Rostam Aziz
Saiod Salim Bakhresa
Reginald Mengi
---
Mfanyabiashara maarufu nchini, Rostam Aziz (49), ametajwa kuwa ndiye tajiri namba moja Tanzania kwa sasa.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Jarida la
Marekani la Forbes na kutoa taarifa yake juzi, Rostam amekamata nafasi
hiyo na ya 27 katika Afrika akiwa na utajiri wa Dola za Marekani bilioni
moja (Sh1.6 trilioni).
Mbunge huyo wa zamani wa Igunga, ameingia kwa mara
ya kwanza katika orodha ya matajiri 50 wa Afrika ya jarida hilo, pamoja
na wafanyabiashara wengine wa Tanzania, Reginald Mengi na Mbunge wa
Singida Mjini (CCM), Mohamed Dewji ‘Mo’. Katika orodha hiyo pia yumo
Said Bakhresa ambaye aliwahi kutajwa siku za nyuma.
Rostam, ambaye aliachana na siasa mwaka
2011,
amempiku Bakhresa, ambaye mwaka jana Jarida la Ventures Africa la
Nigeria lilimtaja kuwa ndiye aliyekuwa tajiri namba moja wa Tanzania.
Bakhressa katika kipindi hicho alikadiriwa kuwa na utajiri wa Dola 620
milioni (Sh971 bilioni).Katika orodha hiyo ya Ventures Africa, Bakhresa
alifuatiwa na Rostam, Mengi na mfanyabiashara mwingine maarufu, Ali
Mufuruki.Kwa habari zaidi Bofya na Endelea......
No comments:
Post a Comment