Header Ads

UJUMBE WA WIZARA YA MAJI NA MISITU TOKA UTURUKI WATEMBELEA OFISI YA MAKAMU WA RAIS.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bwana Sazi Salula akiongea na Ujumbe wa wageni toka wizara ya Maji na Misitu toka nchini Uturuki ofisini kwake mtaa wa Luthuli  leo (picha na mpiga picha maalum).
==========  =========  ==========
UJUMBE WA WIZARA YA MAJI NA MISITU TOKA UTURUKI WATEMBELEA OFISI YA MAKAMU WA RAIS.

      Ujumbe wa wizara ya Misitu na Maji ya nchini Uturuki umewasili Tanzania kwa ziara ya siku saba kuanzia tarehe 29/10-6/10/2013. Ujumbe huo wa watu sita ukiongozwa na Naibu Katibu mkuu wa wizara hiyo Bwana Mahir Kucuk ulitembelea Ofisi ya Makamu wa Rais na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu Bwana Sazi Salula.

         Akiongea na Bwana Salula naibu Katibu mkuu wa wizara ya misitu Uturuki alisema ziko  njia mbalimbali zitakazoweza kutumika kwa wananchi Watanzania ili kupunguza uharibifu wa misitu ambapo wananchi wengi hutumia nishati ya mkaa kama chanzo cha nishati. Katibu Mkuu Bwana Sazi Salula alimuomba asaidie wananchi wa Tanzania kuelewa chanzo kingine cha nishati mbali ya mkaa sababu wengi ya wananchi hasa wa vijijini hutumia mkaa na kuni kama chanzo cha nishati.

        Bwana Mahir Kucuk  alisema kwamba wanaandaa mafunzo endelevu amabayo yatawasaiidia wananchi kutumia majiko yanayotumia kuni chache kwa ajili ya kupikia akaongeza hatua hii itapunguza kabisa ukataji ovyo wa misitu. Alisema kwa Nchini Uturuki wananchi wa hali ya chini hutumia gesi asilia pamoja na majiko yanayotumia kuni chache.

        Ujumbe huo ulitoa zawadi mbalimbali kwa ofisi ya Makamu ya Rais ikiwamo Vitabu na sahani . Baada ya kumaliza ziara katika ofisi ya Makamu wa wa Rais wataendelea pia na ziara katika mikoa ya Morogoro, Dodoma  na Shinyanga.

No comments:

Powered by Blogger.