Header Ads

VIDEO: HIVI NDIVYO AL SHABAAB WALIVYOSHAMBULIA ENEO LA WESTGATE MALL NA MAJINA YA MAGAIDI WALIO NDANI YA JENGO





Jumamosi takriban saa tano na nusu asubuhi, genge la
kigaidi linaloshukiwa kuwa la Al Shabaab lilipata kungia katika eneo la
kibiashara la Westgate wakiwa kwenye magari ya kibinafsi. 



Kundi hilo la takriban watu 10-15 liliweza kuingia kupitia
lango kuu la jumba hilo huku lingine likiingia kutoka eneo la kuegeshea
magari lililoko paani.




Katika lango kuu walianza kwa kumuua mkurugenzi wa kampuni
ya usalama inayolinda eneo hilo kabla ya kuelekea paani ambapo ulikuwa
na hafla iliyoandaliwa na idhaa ya East FM.
 

Wale walioingilia lango kuu wakafululiza hadi duka la Nakumatt lililoko
katika jengo hilo na ni hapa ambapo mauaji ya Wakenya wasiokuwa na
hatia yoyote yalipoendelezwa zaidi.



 

Milio ya risasi ikasheheni angani. Huku
haya yakijiri tayari maafisa wa polisi walikuwa wamepata habari hizo na
vikosi mbali mbali vikakita kambi na kulizingira eneo hilo, magharibi,
mashariki, kusini na hadi angani.

Shughuli ya uokozi ikaanza ili kufanikiwa kuwashikilia
mateka kwa siku tatu mtawalia huku vikosi vya usalama vinajua ina maana
kuwa magaidi hawa walikuwa wamejihami vilivyo.

Na je ni akina nani hawa ?  
Duru za kuaminika zinaarifu kuwa, washukiwa hawa ni watu wa tabaka na
mataifa mbali mbali wakiwemo wafuatao wanaodaiwa kushiriki kwenye
shambulizi hilo:
   
 1. Sayd Nuh – 25 – Kismayu 
 2. Ismael Galed – 23 – Finland  
 3. Mustafa Noordiin – 24 –  Marekani  
 4. Abdifatah Osman- 24 – Marekani
 5. Kassim Musa – 22 – Garissa 
 6. Mohammed Badr – 24 – Syria

Aidha waziri wa masuala ya ndani na usalama Joseph Ole Lenku
amefutilia mbali madai kuwa kiongozi wa kundi hilo ni mwanamke
akishikilia kwamba ni wanaume waliovalia mavazi ya kike.

Kufikia sasa  vikosi vya kenya vya usalama vimechukua
usukani wa orofa zote za jengo hilo, na kulingana na Lenku ni kuwa
magaidi wangali wamejificha, japo wawili tayari wameuawa.

No comments:

Powered by Blogger.