UBALOZI WA TANZANIA NCHINI MAREKANI UNABAGUA VYOMBO VYA HABARI AU AFISA HABARI WAKE NDIYE ANAYEBAGUA?
Na Alex Kassuwi wa Swahili TV na Swahili Radio Online.
Wiki
iliyopita baada ya kulemewa na maswali kutoka
kwa wasomaji,wasikilizaji, watazamaji na wafuatiliaji wa vyombo vyetu
vya habari vya MMK MEDIA GROUP watu wengi sana walituuliza "kwa nini
Swahili TV na Radio hawakuwepo katika tukio kubwa la kihistoria
lililofanyika jumatano ya sept 18, 2013 katika ubalozi wetu wa Tanzania
nchini Marekani, ambapo Mabalozi wa Heshima (Honorary Consuls) walisaini
mikataba mbele ya Rais wetu Mhe.Jakaya Mrisho Kikwete.
UKWELI NI KWAMBA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI MAREKANI UNABAGUA VYOMBO VYA HABARI AU AFISA HABARI WAKE MINDI KASIGA
Baada
ya tukio hafla hiyo kubwa kupita bila kusita niliandika masikitiko
yangu kwa niaba ya MMK MEDIA GROUP wamiliki wa Swahili TV online,
Swahili Radio Online na Blog hii ya Swahilitv.blogspot.com kuhusiana na
yaliyojitokeza ubalozini.
Leo
hii katika tahariri hii nitaelezea na kufafanua makosa yaliyofanywa na
Ubalozi ama Mindi Kasiga na kwa nini hakupaswa ama hawakupaswa kubagua
vyombo vya habari katika tukio lile. PIA NIMEAMBATANISHA BARUA YA MAMALIKO TOKA KATIKA CHOMBO KINGINE CHA HABARI KWA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI MAREKANI.
HIVI NDIVYO WAANDISHI TULIVYOTENDWA
Mosi;
Mindi alionyesha dharau kwa kuwasiliana na vyombo vya habari kwa ujumbe
mfupi wa email kutokea kwenye iPad yake katika akaunti yake binafsi ya
gmail na badala ya kuandika barua ya kiofisi yenye nembo husika na yenye
kumbukumbu na sahihi husika kama ilivyo kawaida. Kuthibitisha kwamba ni
dharau, Mindi Kasiga alionyesha heshima pekee kwa shirika la habari la
kimarekani VOA (Voice of America) kwa kuwapelekea barua ya kiofisi ya
kuwaalika rasmi iliyozingatia taratibu zote za na sheria za kiofisi.
Pili;
Mindi alisingizia ufinyu wa nafasi kuwa mdogo kwa vyombo vingine vya
habari na huku mwaliko wa VOA ukiwa wazi kwa idadi ya watu wowote wale
watakaopenda na watakaotaka kuhudhuria hafla ile wote walikaribishwa
bila masharti.
Tatu;
Mindi hakupaswa kujiamulia kwa kusema namnukuu "upande wa electronic
media wote mtawakilishwa na jamii production". Swali 1. kwa Mindi hivi
unaelewa nini kuhusu electronic media? au bado umebaki na mtazamo wa
zamani ambapo kulikuwa na print na electronic iliyomaanisha Radio na TV
ambavyo vilikuwa analojia, na tena terrestrial zikirusha matangazo kwa minara na mikonga ya mawasiliano. Swali 2. je, vipi
kuhusu digital media? blogs, Online TV, Online Radio na Websites? hujui
kwamba ndio vyombo vya habari vya leo vyenye wasomaji na wafuatiliaji
wengi? Swali 3. Ni Criteria gani Ubalozi ama Mindi Kasiga waliyotumia
kuiteua Jamii Production kuwakilisha vyombo vingine vya habari katika
tukio la Kitaifa?
Nne; Mindi hukupaswa kuagiza vyombo vya habari vingine vipeleke maswali kwa Jamii production. Nakunukuu "kama
kuna maswali yaelekezwe kwao" Mindi huwezi kuagiza chombo cha habari
kupeleka maswali yake kwa chombo kingine, kisha kile kingine kwenda
kuuliza na kuleta majibu, hii haipo katika dunia ya sasa labda karne
zilizopita. Jiulize ni kama vile Ikulu wana hafla halafu unaagiza TBC
Taifa wapeleke maswali yao ITV halafu ITV wakaulize na kisha kuwaletea
jibu TBC Taifa! uliona wapi hiyo?
BARUA YA MALALAMIKO TOKA KWA MWANDISHI MWINGINE AMBAYO ILITUMWA APRIL 2013 KWENDA UBALOZINI
Na Mubelwa Bandio
Shikamoo Mama Munanka.
Natumai kuwa u-mwema na unaendelea vema na kazi za kila siku hapo ofisini.
Binafsi ni mwema na naendelea na pilika za maisha hapa.
Napenda kutumia nafasi hii kueleza masikitiko yangu kidogo kuhusu hali ninayoona ikitokea kati ya ubalozi na jamii kwa ujumla.
Ntajaribu kufupisha jambo hili linalonisumbua sana
Nimekuwa mmoja wa wanaoletewa
maswali ya “kwanini hamjazungumza na viongozi waliokuja hapo ubalozini”
na kwangu nimepata wakati mgumu hata kufikiria jibu.
NI KWA KUWA HATA MIMI HUJIULIZA SWALI HILO
Nilishawahi kuleta maelezo na hata maoni ya namna ya kusaidiana na ubalozi kuunganisha jamii yetu hapa.
Binafsi naamini kuwa
HAITATOKEA HATA SIKU MOJA, KUKAWA NA UJIO WA WAZIRI AMA RAIS AMA
KIONGOZI YEYOTE WA NCHI KWA DHUMUNI MOJA TU LA KUKUTANA NA WATANZANIA
WAISHIO MAREKANI.
Ina maana, pale wanapopata ziara
za kikazi, ndio wakati muafaka wa kukutana na / ama kuwasiliana nasi
waTanzania tuishio huku (kama alivyofanya Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe.)
SOTE TUNAJUA HILI SI KAWAIDA
Nilipata kuleta WAZO hapo
ubalozini kuwa inapotokea ikajulikana kuna Mheshimiwa anayekuja,
waTanzania katika DIASPORA waelezwe na waweze kutuma maoni kwa mhusika
wa habari hapo ubalozini (kwa njia ya barua pepe), na mheshimiwa akija,
tujumuishe maswali ya wanaDIASPORA na yale yatakayoandaliwa na wadau wa
habari na kufanya mazungumzo nao.
Hii ingekuwa NJIA RAHISI NA MUAFAKA ya kuwasilisha mawazo, maswali na hata dukuduku la mTanzania wa Marekani popote alipo. Lakini badala yake, tumekuwa tukisikia kuwa “walikuwepo” na / ama kuwaona katika MATUKIO na kisha wanaondoka.
Katika hili, NAONA KAMA UBALOZI UMETUANGUSHA KATIKA KUTUUNGANISHA NA WALE WANAOTUONGOZA.
Naamini mjadala na kiongozi
toka Tanzania (iwe ni Townhall meeting ama mahojiano yanayoratibiwa na
ubalozi) ni muhimu kwa jamii yetu Nina
hakika kuwa mikutano ya viongozi wanaokuja wanapokutana na viongozi wa
Jumuiya na / ama vyama haikidhi mahitaji ya waTanzania wote nchini kwa
kuwa wanakutana na viongozi wa Metropolitan waliyopo nao hawakutani na
wanachama wote (hata wenye nia).
Nimeona niwasilishe wazo
langu hili kwa mara ya mwisho nikiamini kuwa utawekwa utaratibu muafaka
wa kuTUMIA VEMA ZIARA HIZI kuweza “kuua ndege wawili kwa jiwe moja” Yaani, ndani ya ziara zao za kikazi, waunganishwe nasi watanzania tulio huku.
Natanguliza shukrani NB: Nimewaambatanisha wanahabari wenzangu wa hapa DMV.
Chanzo:www.changamotoyetu.blogspot.com
mwisho wa barua ya Bandio
NAMALIZIA KWA HILI MUHIMU
Pamoja
na mamaliko ya Mwandishi mwenzetu Mubelwa Bandio bado Ubalozi au Afisa
habari wake hawajajirekebisha na bado kero ziko palepale na vyombo vya
habari. Swali, kwa nini viongozi
wa kiserikali wanapokuja katika ziara za kikazi hapa nchini Marekani
Ubalozi hautoi taarifa kwa vyombo vya habari? na badala yake Ubalozi
unatumia chanzo kimoja cha habari, ambapo mwanahabari mmoja huyo
anatumika ku-brake news za Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
wakati sisi wanahabari wengine tunastukizwa na habari za ujio wa
viongozi walifika lini, wamefanya nini nk toka katika chombo hiki kimoja
na tunabaki tukijiuliza hiki ni chombo binafsi ama kitengo cha Ubalozi?
Tungependa kuwe na Freedom of Speech, na Ushirikishwaji kwa vyombo vya
habari vyote bila kubagua. Vyombo vya habari vipo na vinajulikana na
Ubalozi unavitambua kwani vilishajitambulisha.
No comments:
Post a Comment