MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR MAALIM SEIF SHARIFF HAMAD AWASILI MKOANI RUKWA KUSHIRIKI IJITIMAI YA KIMATAIFA
Makamu
wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Maalim Seif Shariff
Hamad akilakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya
aliopowasili leo tarehe 29 Septemba 2013 katika uwanja wa ndege wa
Sumbawanga kwa ajili kushiriki na kufunga Ijitimai ya Kimataifa
inayofanyika Mkoani Rukwa. Ijitimai ni Semina ya kiislam inayolenga
kuihamasisha jamii kumcha Mungu kwa kufanya matendo mema na kuacha maovu
na machafu.
Kiongozi
wa maandalizi ya Ijitimai ya kitaifa na kimataifa inayofanyika Mkoani
Rukwa Amir Ali Jumanne akimtambulisha Makamu wa Rais wa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad viongozi mbalimbali wa dini
ya kiislam walioshiriki katika maandalizi ya Ijitimai.
Mbunge
wa Jimbo la Sumbawanga Mjini CCM, Aeishi Hillal akiteja jambo na Katibu
Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima wakati wa mapokezi ya
Makamu wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika uwanja wa
ndege wa Sumbawanga.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akimsomea Makamu wa Kwanza wa
Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad
taarifa ya Mkoa wa Rukwa katika Ikulu ndogo ya Sumbawanga.
Makamu
wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Maalim Seif Shariff
Hamad akizungumza mara baada ya kusomewa taarifa ya Mkoa wa Rukwa na
Mkuu wa Mkoa huo Injinia Stella Manyanya. Katika mazungumzo yake
ameshukuru kwa mapokezi mazuri aliyoyapata na kuupongeza Mkoa wa Rukwa
kwa uzalishaji mkubwa wa chakula nchini ambapo ameutaka uongozi wa Mkoa
kujikita zaidi kutafuta masoko ya mazao yanayozalishwa na wakulima.
Ameutaka
pia uongozi wa Mkoa kulipa kipaombele suala la usalama akitolea mfano
yaliyotokea nchini kenya na kuvitaka vyombo vya dola kuimarisha uhusiano
na wanachi katika kuboresha taarifa za ulinzi shirikishi. Aliwaasa pia
wanachi kudumisha mahusiano mazuri yaliyopo nchini kwa kuweka pembeni
tofauti zao za kidini na kusaidia kutoa taarifa inayoashiria uvunjifu wa
amani kwa vyombo vya dola .
Akizungumzia
kongamano la uwekezaji lililofanyika Mkoani Rukwa mwaka jana ameutaka
uongozi wa Mkoa kujitangaza zaidi katika fursa zinazopatikana za
uwekezaji na kufuatilia wawekezaji waliotoa ahadi za kuwekeza Mkoani
Rukwa na kuwawekea mazingira mazuri ya kuwekeza.
Baadhi
ya viongozi wa dini na serikali ya mapinduzi ya Zanzibar walioongozana
na Makamu wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Maalim Seif
Sharif Hamad. Katikati ni Waziri wa Habari wa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar Said Ali Mbarouk. Wengine ni Chief Kadhi wa Zanzibar Sheikh
Khamis Haji Khamis na Imam Sheikh Mziwanda Ngwali.
(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)
No comments:
Post a Comment