Header Ads

KAMPENI YA KITAIFA YA AFYA NA USAFI WA MAZINGIRA SHINYANGA

 Afisa Afya wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Ndg.Mohamed Kiula, akieleza hali ya utekelezaji wa Kampeni ya Afya na usafi wa mazingira katika wilaya ya Kishapu kwa wananchi na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.Ally N.Rufunga  mapema wiki hii alipofanya ziara wilayani hapo katika kijiji cha Bupigi kata ya Uchunga,kukagua utekelezaji wa kampeni hiyo ikiwa ni maagizo ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete kuhamasisha jamii kubadili tabia na mtazamo wa jamii katika kutathmini suala la usafi wa mazingira.
 Wananchi wa kijiji cha Bupigi kata ya Uchunga wilaya ya Kishapu wakifanya zoezi la uchefuaji kwa kuongozwa na Afisa Afya wa Halmashauri hiyo ili kuwahamaisha kubadili tabia ya kujisaidia vichakani hali inayosababisha uchafuzi wa mazingira na hivyo kupata magonjwa ya milipuko kama kuharisha, kipindupindu na matumbo.
 Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa Ally N. Rufunga akiwaeleza umuhimu wa kutunza mazingira wananchi wa kijiji cha Bupigi wilaya ya Kishapu mapema wiki hii alipotembelea kijijini hapo kuona utekelezaji wa kampeni ya kitaifa ya Afya na usafi wa mazingira.
Baadhi ya wananchi katika kijiji cha Nyamilangano wilaya ya Kahama wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga(hayupo pichani),akiwaeleza umuhimu wa vyoo na usafi wa mazingira.


Katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga aliyofanya kwenye Halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Halmashauri ya Mji Kahama pamoja na Halmashauri ya wilaya ya Ushetu ametoa rai kwa wananchi kutizama upya suala la mila na desturi kwa baadhi ya makabila kutotumia choo kimoja na wakwe linasababisha uchafuzi wa mazingira kwani inabidi wakati fulani wakwe kujisaidia vichakani pale wanapotembelewa na wakwe zao. Hivyo amewataka wananchi kuacha mila hizo kwani hakuna madhara yoyote,vinginevyo kaya hizo ziwe na vyoo viwili.

Amewataka pia viongozi hasa Wakuu wa wilaya kusimamia sheria ya uchafu wa mazingira inayomfunga mtu yeyote mwenye kosa hilo kwa mwaka mmoja au faini ya Tsh.Milioni moja.

Mkuu wa Mkoa ametembelea vijiji vya Bupigi wilaya ya Kishapu, Mpunze Halmashauri ya wilaya ya Ushetu na Nyamilangano katika Halmashauri ya Mji Kahama ili kuona hali ya utekelezaji wa kampeni hiyo.

Magdalena Nkulu
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa 
Shinyanga

No comments:

Powered by Blogger.