MH. LOWASSA AONGOZA HARAMBEE YA KUNUNUA BASI LA KWAYA LA KANISA LA KKKT,MSASANI JIJINI DAR
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la
Monduli,Mh. Edward Lowassa akihutubia waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri
Tanzania usharika wa Msasani jijini Dar es Salaam wakati wa sherehe za uzinduzi
wa DVD ya Kwaya na harambee ya ununuzi wa basi la kwaya ya Kanisa
hilo,iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.Mh. Lowassa ambaye aliongozana na
familia yake yote, alichangia shilingi millioni 10, huku wanawe wakitoa kiasi
cha shilingi milioni tano.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la
Monduli,Mh. Edward Lowassa (kushoto) akipongezwa na Mchungaji wa
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania usharika wa Msasani,Eliguard Muro mara
baada ya kuhutubia na kuzingua DVD ya kwaya ya Kanisa hilo na kuendesha Harambee
ya Kuchanfia Ununuzi wa Basi la Kwaya ya Kanisa hilo,iliyofanyika leo jijini Dar
es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Benki ya CRDB,Dk. Charles
Kimei (kulia) akiwahamasisha waumini wengine kujitokeza kuchangia Harambee
hiyo,ambapo yeye binafsi aliweza kuchangia kiasi cha Sh. Milioni 7 katika
harambee hiyo.Kushoto ni Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh.
Edward Lowassa ambaye ndie alieiongoza harambee
hiyo.
Mdau Richard Kasesela akichangia kiasi cha
Dola 300 katika harambee hiyo
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la
Monduli,Mh. Edward Lowassa akijadiliana jambo na Mkewe Mama Regina Lowassa kabla
ya kuanza kwa sherehe za uzinduzi wa DVD ya Kwaya na harambee ya ununuzi wa basi
la kwaya ya Kanisa hilo,iliyofanyika leo jijini Dar es
Salaam.
Mke Waziri Mkuu Mstaafu,Mkewe Mama Regina
Lowassa (kushoto) akiwa na Familia yake wakati wa sherehe za uzinduzi wa DVD ya
Kwaya na harambee ya ununuzi wa basi la kwaya ya Kanisa hilo,iliyofanyika leo
jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment