---
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema) amesema yupo
tayari kuipa Serikali wachunguzi wa kimataifa iwatumie kuchunguza
Watanzania walioficha fedha haramu kwenye Benki za Uswisi.
Kauli hiyo ya Zitto imekuja takriban wiki moja tangu alipoieleza Serikali kwamba kama imeshindwa kuwachunguza walioficha fedha Uswisi, iwaachie wenye uwezo wa kufanya suala hilo yenyewe isubiri majibu kwa manufaa ya nchi.

Zitto ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, alisema kauli ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), George Mkuchika kuwataka Watanzania kupeleka majina ya vigogo walioficha mabilioni kwenye benki hizo ili wachunguzwe, inaingilia uhuru wa Bunge na kwamba alitakiwa kuzungumza jambo hilo bungeni.Kwa habari zaidi
No comments:
Post a Comment