MAKAO MAKUU YA CCM DODOMA WAMPOGEZA JK, SEKRETARIETI
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwasili kwenye viwanja vya
Ofisi za Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma leo, katika hafla fupi ya
kumpongeza kwa kuchaguliwa tena kuwa Mwenyekiti wa Chama, juzi. Kushoto
ni Mama Salma Kikwete, Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana na wanne
ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba.
MAMBO HAYA SI MCHEZO: Katibu Mkuu wa UVCCM, Martine Shigella anaonekana
ndovyo alivyokuwa akisema, wakati alipokuwa kibadilishana mawazo na
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba na Katibu wa NEC,
Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakati wa hafla hiyo.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, akibadilishana mawazo na
wasaidizi wake, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula na Katibu
Mkuu wa CCM, Abdurahman Kinana wakati wa hafla hiyo.
Baadhi ya wanachama wa CCM waliohudhuria hafla hiyo, wakishangilia
Wasanii wakitumbuiza ngoma ya Kigogo wakati wa hafla hiyo. (Picha zote na Bashir Nkoromo)





No comments:
Post a Comment