Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe azungumza na Mabalozi wa Nje nchini
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (katikati),
akizungumza masuala mbalimbali na Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika
ya Kimataifa hapa nchini, Dar es Salaam leo, ukumbi wa Karimjee,
jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Balozi Juma Mpango wa Kongo (DRC),
ambaye pia ni kiongozi wa Mabalozi wa nje hapa nchini na kulia ni Kaimu
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Rajab Gamaha.
Baadhi
ya Mabalozi, wakiwemo Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini (EU), Filiberto
Ceriani Sebregondi (kulia) na Naibu Balozi wa Ujerumani nchini, Hans
Koeppel (katikati), wakimsikiliza Waziri Membe wakati alipokuwa
akizungumza nao leo katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya Mabalozi, wakiwemo Balozi wa Malawi, Flosie Asekanao
Gomile-Subiaomba (wa tano kutoka kushoto) na Mabalozi kutoka nchi za
Nigeria, Pakistani, Palestina, Rwanda, Somalia na nchi nyingine,
wakimsikiliza Waziri Membe, wakati akizungumza nao leo katika ukumbi wa
Karimjee jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (katikati),
akizungumza masuala mbalimbali na Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika
ya Kimataifa hapa nchini leo katika ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es
Salaam. Kushoto ni Balozi Juma Mpango wa Kongo (DRC), ambaye pia ni
kiongozi wa Mabalozi wa nje hapa nchini na kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo, Balozi Rajab Gamaha. (Picha zote na Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa)




No comments:
Post a Comment