Mbeki asema mapatano yamepatikana Sudan
Mpatanishi
wa Umoja wa Afrika, Thabo Mbeki, ametangaza mapatano baina ya Sudan na
Sdudan Kusini kuhusu malipo ya mapato ya mafuta baada ya mzozo wa
miezi kadhaa, ambao ulikaribia kuingiza mataifa hayo mawili vitani.
Bwana
Mbeki aliwaambia waandishi wa habari katika mji mkuu wa Ethiopia,
Addis Ababa, kwamba maswala yote yaliyokuwa yamebaki, sasa
yametatuliwa, lakini hakutoa maelezo zaidi.
Sudan na jirani yake hawakusema kitu hadi sasa.
Sudan Kusini ilisitisha usafirishaji wa mafuta kupitia Sudan mwezi wa Januari, kufuatia mzozo kuhusu ada iliyokuwa ikitozwa na serikali ya Khartoum.
Sudan na jirani yake hawakusema kitu hadi sasa.
Sudan Kusini ilisitisha usafirishaji wa mafuta kupitia Sudan mwezi wa Januari, kufuatia mzozo kuhusu ada iliyokuwa ikitozwa na serikali ya Khartoum.
No comments:
Post a Comment