KCB YAMWAGA MISAADA ZANZIBAR
Katibu
Mkuu wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar,Bw.Omar Abdallah akipokea
msaada wa vyandarua pamoja na mashine ya kupumlia wagonjwa(Oxygen
Conamtrator)vyenye thamani ya Milioni Tano kwa niaba ya Hospitali ya
Mwembeladu kutoka kwa Meneja wa banki ya KCB Tawi la Stone Town
Zanzibar Bw.Rajabu Ramia.Kulia ni Meneja wa Biashara wa Benki ya KCB
Zanzibar Bw.Abdallah Mshangama.
Katibu
Mkuu wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar,Bw.Omar Abdallah kushoto
akipokea Mashine ya kupumlia wagonjwa(Oxygen Conamtrator) kwa niaba ya
Hospitali ya Mwembeladu kutoka kwa Afisa Uhusiano wa Benki ya KCB Tawi
la Stone Town Zanzibar Bw.Said Amour,katikati Meneja wa banki ya KCB
Tawi la Stone Town Zanzibar Bw.Rajabu Ramia,Benki hiyo ilitoa msaada wa
vifaa vyenye thamani ya Shilingi Milioni Tano.
Meneja
wa Benki ya KCB Tawi la Stone Town Zanzibar Bw.Rajabu Ramia,akimkabidhi
Muuguzi Msaidizi wa Hospitali ya Mwembeladu Zanzibar Bi.Zawadi Suleiman
Msaada wa Vyandarua pamoja na mashuka 50 na vifaa mbalimbali vyenye
jumla ya thamani ya Shilingi Milioni Tano.
Afisa
Mahusiano wa Benki ya KCB Tanzania Bi. Martha Edward akimpatia zawadi
ya Tende Bi.Amina Ahamed alielazwa katika Wodi ya Wazazi kwenye
Hospitali ya Mwembeladu Zanzibar mara baada ya wafanyakazi wa Benki ya
KCB kufika katika Hospitali hiyo kwa lengo la kutoa msaada wa vifaa
mbalimbali vyenye jumla ya thamani ya Shilingi Milioni Tano.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Benki ya KCB wakiwa kwenye picha ya pamoja na wauguzi
wa Hospitali ya Mwembeladu Zanzibar mara baada ya wafanyakazi wa Benki
hiyo kufika katika Hospitali hiyo kwa lengo la kutoa msaada wa vifaa
mbalimbali vyenye jumla ya thamani ya Shilingi Milioni Tano.





No comments:
Post a Comment