MAADHIMISHO YA SIKU YA KUMBUKUMBU YA MASHUJAA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA JIJINI DAR ES SALAAM LEO
Rais Dkt. Jakaya Kikwete, akiweka Ngao na
Mkuki kwenye Mnara wa Mashujaa, wakati wa maadhimisho ya siku ya
kumbukumbu ya Mashujaa, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja
jijini Dar es Salaam, leo.
Mkuu wa Majeshi, Davis Mwamunyange akitoka kuweka silaha ya jadi
kwenye Mnara wa Mashujaa, wakati wa maadhimisho ya siku ya kumbukumbu
ya Mashujaa, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es
Salaam, leo.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akiwasili
kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo, kuhudhuria
sherehe za maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, leo.
Kutoka
(kushoto) Rais Dkt. Jakaya Kikwete, Mkuu wa Majeshi, Davis
Mwamunyange, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
Mohammed Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu
wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd, Rais Mstaafu wa awamu ya
pili, Ali Hassan Mwinyi, Spika
wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho....., Waziri wa
Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha na Mkuu wa Mkoa
wa Dar es salaam, Said Meck Sadiq, wakiwa katika viwanja vya Mnazi Mmoja wakihudhuria sherehe za maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, leo.
Sehemu ya wageni waalikwa na Mabalozi wa nchi mbalimbali waliohudhuria maadhimisho hayo.
Askari wa Jeshi wakishiriki katika maadhimisho hayo, hapa wakiweka silaha begani.
Ni ishara ya kutoa heshima kwa Mashujaa wapiganaji.
Rais
Dkt. Jakaya Kikwete, akisalimiana na baadhi ya wazee waliopigana vita
mbalimbali vya ukombozi wa nchi ya Tanzania, waliohudhuria katika
maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, iliyofanyika kwenye
Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akisalimiana na baadhi ya wazee waliopigana vita mbalimbali vya
ukombozi wa nchi ya Tanzania, waliohudhuria katika maadhimisho ya siku
ya kumbukumbu ya Mashujaa, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja
jijini Dar es Salaam, leo.
Huyu ni Mzee CUF, ni maarufu kwa upigaji picha za kuuza 'BANYAA' huyu
pia ni miongoni mwa wapiganaji ambao walipata kupigania haki ya
Mtanzania wa leo enzi hizo, ambaye kwa sasa kazi yake kubwa ni
kujishughulisha na uuzaji wa picha katika shughuli mbalimbali, hapa
akihaha kusaka matukio ya kuweka katika karatasi ya picha zake ambazo
baadaye atafanya biashara. Mzee huyu baada ya kuona siku ya leo ni
muhimu hata kwake pia lakini akiweka kazi yake mbele zaidi ili
kujipatika kipato alionelea ni vyema naye pia akakumbukia mavazi yake
haya aliyoyavaa na kutinga nayo eneo la tukio ili kuepuka kusumbuliwa
na wahusika aweze kuingia kirahisi eneo la tukio kama unavyomuona akiwa
bize na vazi lake huku akiwa na begi kubwa la kamera wakati
kajikamera alikonako ni kibiriti. Hii yote ni janja tu ilimradi mkono
uende kimiani.
Mzee CUF, akiwa bize kunasa picha za wajeda wakiwa katika paredi,
begani ni bonge la begi la kamera ambalo ndani yake halina
kilichokusudwa.

Mzee CUF bado yu bize........
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, akiomba dua kwa niaba ya waislam wakati wa maadhimisho hayo leo.
Kiongozi wa dini ya kikristo, Mchungaji Kamoyo, akiomba sala kwa niaba ya wakristo wakati wa maadhimisho hayo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akiagana na wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, wakati
akiondoka kwenye uwanja wa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo baada
ya kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa.














No comments:
Post a Comment