IGP UGANDA AAGIZA MAAFISA UBALOZI WA TANZANIA NCHI UGANDA WAILETE HARAKA SANA PASSPORT YA MSANII WA UGANDA JOSE CHAMELEON
Mkuu
wa jeshi la polisi nchini Uganda, IGP, Kale Kayihura amewaagiza
maofisa wa Tanzania kuirudisha haraka passport ya Jose Chameleone.
Kayihura ametoa amri hiyo alipokutana na Chameleon kwenye kituo cha polisi cha Muyenga mchana wa leo jijini Kampala.
Amesema maafisa wa hapa nchini wamesema passport ya msanii huyo ingewasili baadaye leo na kukabidhiwa kwake mara moja.
Leo
Jose Chameleone akiwa na mashabiki wake wameandamana kwenye ubalozi wa
Tanzania nchini Uganda kudai arudishiwe passport hiyo iliyokuwa
ikishikiliwa na Erick Shigongo kwa madai kuwa meneja wake amemtapeli
dola 3500.

No comments:
Post a Comment