Makamu wa Pili wa Rais Wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Atoa Mkono Kwa Wananchi Waliopoteza Nyumba Zao Kwa Ajali Ya Moto Huko Mchekeni Kiwengwa Zanzibar
Makamu
wa Pili wa Rais Wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi shilingi
laki nne {400.000/- } sheha wa Shehia ya Kiwengwa Bwana Maulidi Masoud
ame kwa ajili ya kuwafariji wananchi wa mchekeni ambao nyumba zao nane
zimeteketea kwa moto jumamosi jioni ya terehe 18/2/2012.katikati ni mkuu
wa mkoa wa Kaskazini Unguja Mh. Pemba Juma Khamis.
Makamu
wa Pili wa Rais Wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na baadhi
ya wakaazi wa mchekeni kiwengwa ambao nyumba zao zimeteketea kwa moto.
Kushoto yake ni mkuu wa wilaya Ya Kaskazini B Nd. Vuai Ali Vuai, kulia
ya balozi ni mkuu Wa Mkoa Kaskazini Unguja Mh. Pembe Juma Khamis na
pembeni ni balozi wa nyumba kumi Mchekeni nd. Elyas Yaqoub
Mabaki
ya Viwanja vya Nyumba Nane zilizoteketea kwa Moto katika maeneo ya
Kiwengwa Mchekeni juzi, na kusababisha Familia za nyumba hizi kukosa pa
kukaa kutokana na janga hilo la moto ulioazia katika moja ya nyumba
hizo.
Wasamaria wema wakitowa msada wa kuokoa mali za Wananchi waliounguliwa na Nyumba zao.
Wanafamilia wakiwa wameduwaa baada ya kupata baadhi ya mali zao na nyengine kuteketea kwa moto.
--
Serikali
itaangalia hali halisi ya namna gani itakavyotoa maamuzi muwafaka
kuhusiana na Wananchi wanaoishi kwenye eneo lililotengwa kwa hifadhi ya
Misitu liliopo Kiwengwa Pongwe.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameeleza hayo wakati akitoa mkono wa pole kwa Familia nane za Wananchi waliokumbwa na janga la nyumba zao kuteketea kwa moto hapo Mchekeni Kiwengwa Wilaya ya Kaskazini ‘‘B’’.
Familia Tano za Wananchi hao hivi sasa zimehifadhiwa katika Jengo la Ofisi ya CCM Jimbo la Kitope iliyopo Kinduni na Tatu zilizobaki zimepata hifadhi kwa Majirani wa karibu wa Eneo hilo la Mchekeni.
Balozi
Seif alisema ni vyema kwa Serikali ikatafakari kwa pamoja suala la
Makaazi ya Wananchi hao sambamba na umuhimu wa hifadhi ya Misitu iliyopo
katika sehemu hiyo.
“ Maamuzi yoyote yatakayotolewa na Serikali lazima myakubali. Inawezekana kuhamishwa au kuendelea kubakia hapa, lakini cha msingi zaidi ni kutolewa uwamuzi utakaolinda maslahi zaidi ya jumla ya Taifa ”. Alisisitiza Balozi Seif.
“ Maamuzi yoyote yatakayotolewa na Serikali lazima myakubali. Inawezekana kuhamishwa au kuendelea kubakia hapa, lakini cha msingi zaidi ni kutolewa uwamuzi utakaolinda maslahi zaidi ya jumla ya Taifa ”. Alisisitiza Balozi Seif.
“ Hivi sasa wapo tu kama popo hawana uwezo wa kujenga makaazi ya kudumu kwa sababu eneo hilo kutangazwa kuwa Hifadhi ya Misitu ”. Balozi Seif aliendelea kufafanua zaidi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwaeleza Wananchi hao kwamba lazima wawe na uhakika wa Maisha yao yakiambatana pia na shughukli zao za Kimaisha kama vile Kilimo na harakati za ujasiri amali.
Alisisitiza kwamba Wanakijiji hivi sasa wanashindwa na maamuzi ya ujenzi wa nyumba za kudumu kutokana na Mamlaka inayohusika na misitu kutoruhusu ujenzi katika eneo hilo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akiwa pia ni Mbunge wa Jimbo la Kitope alitoa mchango wa Shilingi Laki Nne kuwafariji Wananchi hao kutokana na Janga hilo ili kupata kianzio cha Maisha.
Mapema Mjumbe wa Nyumba Kumi { Balozi } katika eneo hilo Nd. Elyas Yaqoub alimueleza Balozi Seif kwamba chanzo cha Moto huo ni Mtoto wa moja ya Familia zilizopata janga hilo kujaribu kusaidia harakati za mapishi kwenye nyumba yao na baadaye kushindwa kudhibiti moto aliokuwa akiuchochea jikoni hapo.
Naye Sheha wa Shehia ya Kiwengwa Bwana Maulid Masoud Ame alisema Wakaazi wa eneo hilo wanalazimika kuendelea kujenga nyumba za Makuti ambazo ni hatari kwa vile eneo hilo liko katika msongamano wa mawazo.
Bwana
Maulid Alisema mbali ya suala hilo lakini hata huduma za maji zimekuwa
finyu na kupelekea Wananchi hao kushindwa kukabiliana na Moto huo
kutokana na ukosefu wa Maji.
Nyumba nane zilizoungua moto huo zilikuwa zikimilikiwa na Nd. Six Alfred, Kisumo Paulo, Maganga Said, Chales Lukas, Stephano Kabangara, Simon Chales, Tabia Petro na Mwashi Kabangara.
Nyumba nane zilizoungua moto huo zilikuwa zikimilikiwa na Nd. Six Alfred, Kisumo Paulo, Maganga Said, Chales Lukas, Stephano Kabangara, Simon Chales, Tabia Petro na Mwashi Kabangara.
Hadi sasa hasara ya gharama ya jumla iliyotokana na kuunguwa kwa Nyumba hizo bado haijajuilikana ambapo baadhi ya Wakaazi hao wamepoteza kila kitu.
Na
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
No comments:
Post a Comment