Header Ads

UGANDA YADHAMIRIA KUPITISHA SHEHENA ZA MIZIGO KUPITIA BANDARI YA DAR ES SALAAM

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 

WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi wa Uganda, Mhandisi Monica Mtege amesema, nchi hiyo imedhamiria kupitisha shehena nyingi za mizigo yao katika bandari ya Dar es Salaam kwa sababu ya vivutio vingi vilivyopo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana mara baada ya kufanya ziara katika bandari ya Dar es Salaam Mhandisi Mtege amesema bandari hiyo ni njia rahisi kwao ya kupitisha mizigo yao na pia usafiri wa kutumia njia ya maji ni wa bei nafuu.Alisema vivutio vilivyopo katika bandari ya Dar es Salaam hawaoni sababu itakayo wakwamisha kupitisha mizigo yao na kuendeleza uchumi wa nchi yao.

" Kufika Bandari ya Dar es Salaam ni mara yangu ya kwanza lakini nimeshuhudia mambo mengi ikiwamo maboresho ya miundombinu hivyo napongeza Serikali ya Tanzania ambazo zimechukuliwa hasa za kufungua njia ya ukanda wa kati jambo lililorahisisha kufika kwa mizigo kutoka Dar es Salaam kwenda Uganda," alisema Monica.

Amesema tayari wamejiandaa kuhakikisha wanasafirisha shehena kwa wingi kutoka Uganda kuja Dar es Salaam.Amesema tayari wameandaa makampuni makubwa yenye nia ya kuja Dar es Salaam kupitia njia ya ukanda wa kati.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Masoko wa TPA, Lydia Malya amesema, tayari bandari wameanzisha kikosi kazi maalum ili kuhakikisha wanapata mizigo mingi zaidi ya Uganda.Amesema watatumia fursa mbalimbali kutangaza njia hiyo kwa faida ya nchi mbili.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Uganda, Mhandisi Monica Mtege akizungumza katika mkutano wa menejimenti ya TPA wakati alipotembelea bandari hiyo jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano-Uchukuzi na Mawasiliano, Dk. Leonard Chamuriho akitoa maelezo wakati  Waziri wa Uganda alipotembelea banadari ya Dar es Salaam
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Banadari , Mhandisi Karim Mataka akizungumza wakati wa ziara ya Waziri wa ujenzi na Uchukuzi wa Uganda alipotembelea Bandari ya Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Profesa Ignatus Rubaratuka akizungumza kuhusiana na mamlaka hiyo kuhakikisha inatoa huduma bora kutokana na ushirikiano kati ya Uganda na Tanzania

No comments:

Powered by Blogger.