Header Ads

Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe Omar Yussuf Azinduzi wa Tawi la Bank Of Africa Mlandege Zanzibar.

uzinduzi huo umefanyika katika eneo la Bank hiyo Mlandege Zanzibar. Na kuwataka Wafanyakazi na Uongozi wa BOA kutowa huduma bora na kuwafikia Wananchi wa Vijijini katika kutowa huduma zao.  
Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe Omar Yussuf mwenye mkasi akijiandaa kukata utepe kuashiria kulizindua Tawi la Bank Of Africa Zanzibar lilioko katika barabara ya Mlandege.kushoto Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Balozi Mwanaidi Maajar. 
Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe Omar Yussuf Mzee na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bank Of Africa wakishiriki katika kukata utepe kulizindua rasmin Tawi la Bank Of Africa Zanzibar, uzinduzi huo umefanyika Zanzibar. 
Wageni Waalikwa na Wajumbe wa Bodi na Maofisa wa Bank Of Africa wakishangilia Uzinduzi huo wa Tawi lao la Banki Zanzibar.
Wageni Waalikwa na Wananchi wakihudhuria hafla hiyo.
Maofisa wa Bank Of Africa wakifuatilia uzinduzi wa Bank yake Zanzibar uliofanywa na Waziri wa Fedha Mhe Omar Yussuf Mzee.

Wajumbe wa Bank Of Africa wakiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Bank Of Africa Nchini Tanzania Bwa. Ammish Owusu-Amoah, katikati wakizungumza wakimsubiri Mgeni rasmin Waziri wa Fedha Zanzibar.
Mwenyekiti wa Bodi ya Bank Of Africa Tanzania Balozi Mwanaidi Maajar akisalimiana na Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe Omar Yussuf Mzee alipowasili katika viwanja vya Bank hiyo hapo mlandege kwa ajili ya Uzinduzi wa Bank hiyo.
Waziri wa Fedha Zanzibar akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya Bank Of Africa alipowasili katika eneo hilo. akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya BOA, Balozi Mwanaidi Maajar.

No comments:

Powered by Blogger.