Ziara ya Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Eng.Edwin Ngonyani
(katikati) akielekezwa jambo na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Bw.Magid
Hemed alipofanya ziara yake ya kutembelea Wilaya hiyo kwa kuangalia
mradi wa ujenzi wa daraja la Ruvu chini na bandari ya Bagamoyo.
Naibu
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Eng.Edwin Ngonyani
(katikati) akionyeshwa ramani itakapojengwa bandari ya Bagamoyo kutoka
kwa Msimamizi wa Mradi wa Upanuzi wa Bandari hiyo kutoka Mamlaka ya
Bandari nchini Bw. Alexender Ndibalema (Kushoto) katika ziara yake ya
kutembelea Wilaya ya Bagamoyo.
Eneo ya Chuo cha Uvuvi cha Mbegani Wilayani Bagamoyo ambayo ipo katika mpango wa kubadilishwa na kuwa Bandari ya Bagamoyo.
Naibu
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Eng.Edwin Ngonyani
(kulia) akisalimiana na Mafundi wa kampuni ya Ujenzi ya ESTIM inayojenga
daraja la Ruvu chini katika barabara ya Bagamoyo kwenda Msata katika
ziara yake ya kutembelea Wilaya ya Bagamoyo.
Naibu
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Eng.Edwin Ngonyani
(kulia) akielekeza jambo wakati alipotembelea ujenzi wa daraja la Ruvu
chini katika barabara ya Bagamoyo kwenda Msata , wanaongalia ni Mkuu wa
Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Magid Hemed (katikati) na Kushoto ni Mbunge wa
Bagamoyo Mhe. Shukuru kawambwa.
No comments:
Post a Comment