KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA YAANZA KAZI RASMI – YAPOKEA TAARIFA YA UTENDAJI YA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni akijitambulisha
kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na
Usalama kabla ya Kamati hiyo kuipokea taarifa ya Wizara hiyo katika
kikao cha kwanza cha Kamati hiyo baada ya kuundwa na Bunge hivi
karibuni. Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Balozi Adadi
Mohamed Rajabu anayefuatia ni Makamu wake, Kanali Masoud Khamis. Kulia
kwa Masauni ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest
Rwegasira. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa
Kimataifa wa Kisenga jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi.

Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Balozi
Adadi Mohamed Rajabu akizungumza jambo na Wajumbe wa Kamati yake pamoja
na Watendaji Wakuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika kikao
chao kwanza tangu Kamati hiyo iundwe na Bunge hivi karibuni. Wapili
kulia mstari wa mbele ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia
Hamad Masauni, na kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja
Jenerali Projest Rwegasira. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo,
Kanali Masoud Khamis. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano
wa Kimataifa wa Kisenga jijini Dar es Salaam leo. Picha na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi.

Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni akitoa taarifa
ya Wizara katika kikao cha kwanza cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo
ya Nje, Ulinzi na Usalama. Kikao hicho kilichohudhuriwa na Wajumbe wa
Kamati hiyo pamoja na Maafisa wa Wizara, kilifanyika katika Ukumbi wa
Mikutano wa Kimataifa wa Kisenga jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Balozi Adadi Mohamed Rajabu. Picha na Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


No comments:
Post a Comment