TAMASHA LA MADIVA KUFANYIKA DISEMBA 4 MWAKA HUU MKOANI MBEYA
Msanii
wa kizazi kipya Vanessa Mdee (Wa pili kushoto) akiwa kwenye picha ya
pamoja na madansa wake wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Trust “Divas
Only” lililofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dodoma. Tamasha hilo ni
mahususi kwa utoaji elimu ya uzazi wa mpango kwa kina dada ambalo
liliratibiwa na Shirika la DKT international.
Msanii
Vanessa Mdee (kushoto) akibadilishana mawazo na wafanyakazi mbalimbali
wa Shirika la DKT International kabla ya kufungua rasmi Tamasha la Divas
Only ambalo lilifanyika jijini Dodoma mwishoni mwa wiki. (Katikati) ni
Meneja Masoko DKT International Sialouise Shayo.
Kaimu
meneja wa DKT International tawi la Dodoma Bi.Zena Mgoi akitoa elimu ya
uzazi wa mpango kwa kina dada waliohudhuria uzinduzi wa Tamasha la
“Divas Only” ambalo lililofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dodoma.
Mwishoni
mwa wiki TRUST wazindua mfululizo wa matamasha ya kusisimua ya Divas
Only ambayo yalimshirikisha mwanadada na msanii wa muziki wa kizazi
kipya Vanessa Mdee.
Trust
ni chapa ya njia za kisasa za uzazi wa mpango zenye kuaminika pamoja na
bidhaa na huduma za maisha na urembo zinazotengenezwa na wanawake kwa
ajili ya wanawake.
Trust
ipo ili kuhamasisha madiva wajipange kwa ajili ya baadaye,Madiva wa
Trust wanataka kufanya maamuzi na kupanga kwa ajili ya mafanikio, Trust
iko hapa kukusaidia wakati wa safari hii.
Tulifurahia
muda tuliopata kukaa na Vanesaa na Madiva wa Trust wa Dodoma, Kama wewe
ni Diva wa Trust ama unataka kujua Trust inahusu nini, njoo ukutane na
Madiva wa Trust wengine pamoja na Vanessa Mdee katika matamasha yetu
mengine Mbeya Desemba 04 pale Sunset Hall, Soweto na Mwanza Desemba 13,
Malaika Beach Resort. Huwezi kufika? Tafuta eneo lilipo Dodoma, Mbeya na
Mwanza katika tovuti yetu (trustlife.co.tz) na ututembelee leo!

No comments:
Post a Comment