SERIKALI YAKANUSHA KUHUSU HAZINA KUACHWA TUPU

Kamishna wa Bajeti kutoka Wizara Fedha Bw. John Cheyo akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu kubadilishwa kwa matumizi ya Fedha za Serikali ambazo zitaelekezwa kwenye shughuli zitakazowagusa wananchi ikiwemo uboreshaji wa sekta ya elimu ambapo awali fedha hizo zilipangwa kutumika katika sherehe za Uhuru na shughuli zisizo za lazima. Kulia ni Mkurugenzi msaidizi Idara ya Habari. (MAELEZO) Bw. Vicent Tiganya.




Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Wizara ya
Fedha na vyombo vya habari ambapo Kamishna wa Bajeti kutoka Wizara hiyo
Bw. John Cheyo alitoa ufafanuzi kuhusu utekelezaji wa bajeti ya Serikali
kulingana na mipango iliyowekwa katika kuwahudumia wananchi.Picha na frank Mvungi- Maelezo
--

Na Jovina Bujulu-Maelezo
Serikali imekanusha taarifa zinazosambazwa na baadhi ya vyombo vya
habari kuwa Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuwa
amekomba fedha hazina na kuiacha Serikali bila fungu lolote.
Hayo yamesemwa jijini dare es salaam na Kamishina wa Bajeti kutoka
Wizara ya Fedha Bwa. John Cheyo huku akiwataka wananchi kupuuza habari hiyo
kwani hazina ukweli wowote.
“Hazina inazo pesa za kutosha na tunajivunia kufanya
uchaguzi wa mwaka huu, kununua mashine za BVR kwa kutumia pesa za
watanzania bila kutegemea msaada wowote kutoka nje ya nchi na kutoa
mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu mwaka huu” alisema Bwa. Cheyo.
Pia aliongeza kuwa serikali imeendelea kugharamia miradi
mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa bomba la gesi ambalo limekamilika
hivi karibuni, vinu vya kuchakata gesi na ujenzi wa barabara nchini.
Aliendelea kusema kwamba mfumo wa serikali wa bajeti unaiwezesha
serikali kupanga vipaumbele vya matumizi kulingana na bajeti ilivyopangwa
ambapo fedha zinazokusanywa kupitia mfuko mkuu wa serikali ndizo hutumika.
Bajeti iliyoidhinishwa na Bunge kwa kipindi cha 2015-2016 ni
shilingi Trilioni 22.5 na bajeti hiyo inatengenezewa mpango wa makusanyo na
matumizi kwa kulipia mishahara ya wafanyakazi na miradi mbalimbali
iliyoidhinishwa.
Pia katika matumizi mengine bajeti hiyo inalipia chakula cha
wanafunzi, mikopo ya wanafunzi elimu ya juu, ununuzi wa dawa na vifaa tiba na
chakula cha hifadhi ya taifa.
No comments:
Post a Comment