UMEME WA GESI ASILIA KUANZA KUTUMIKA HIVI KARIBUNI
Waziri
wa nishati na madini George Simbachawene akiwa na wajumbe wa Tanesco
akitembelea miradi ya umeme wa gesi alisilia iliyogunduliwa Mtwala,
katika kituo lilichojengwa na Kampuni ya mafuta ya Tanzania Petrolium
Development Corpolation (TPDC) hii ni sehemu iliyojengwa ni kituo
kikubwa cha kutunzia gesi ya kutengenezea umeme katika kituo cha
Kinyerezi jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi
mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dk.James
Mataragio akizungumza na waandishi wa habari katika katika ziara ya
waziri wa nishati na madini George Simbachawene, kukagua miradi ya umeme
wa gesi asilia katika kituo kikubwa cha kufikia gesi asilia kilichopo
kinyerezi jijini Dar es Salaam leo.
Waziri
wa Nishati na Madini,George Simbachawene akizungumza na waandishi wa
habari leo katika kituo cha kufikia gesi asilia inayotoka Mtwala ili
iweze kutengeneza umeme kutokana na umeme wa maji kupungua kutokana na
vyanzo vya maji vya mto Mtera na Kihansi kupungua maji kwaajili ya
mabadiliko ya hali ya hewa.Kushoto ni Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la
Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dk.James Mataragio.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
No comments:
Post a Comment