TPB YAZINDUA RASMI KADI YA ATM KWA KIKUNDI CHA VICOBA ENDELEVU
Rais wa VICOBA Endelevu, Devota Likokola,
(Watatu kushoto), akinyanyua juu, mfano wa ATM kadi ya Benki ya Posta Tanzania,
TPB, wakati wa uzinduzi wa kadi hiyo itakayotumiwa na wanachama wa VICOBA
Endelevu kota nchini. Uzinduzi huo ulifanyika leo Agosti 15, 2015 kwenye bustani
ya kumbukumbu ya mashujaa, Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Moses Manyanta, Mwenyekiti wa Bodi wa Wadhamini ya Benki hiyo, Profesa Lettic Rutashobya, na Katimu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezweshaji Wananchi Kiuchumi, NEEC, Beng’ Issa.(Picha na Habari na K-VIS MEDIA)
Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Moses Manyanta, Mwenyekiti wa Bodi wa Wadhamini ya Benki hiyo, Profesa Lettic Rutashobya, na Katimu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezweshaji Wananchi Kiuchumi, NEEC, Beng’ Issa.(Picha na Habari na K-VIS MEDIA)
BENKI
ya Posta Tanzania, TPB, imezindua rasmi kadi maalum ya ATM kwa ajili ya
wanachama wa kikundi cha, VICOBA Endelevu.
Hafla
ya uzinduzi huo ilifanyika kwenye bustani ya kumbukumbu ya Mashujaa, Mnazi
Mmoja jijini Dar es Salaam, Agosti 15, 2015, ambapo Mwenyekiti wa Bodi ya
Wadhamini ya TPB, Profesa Lettic Rutashobya, ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi,
pamoja na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi,
(NEEC), Beng’ Issa, walishuhudia Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Moses
Manyanta, akimkabidhi mfano wa kadi hiyo ya ATM, Rais wa Vicoba Endelevu,
Devota Likokola mbele ya mamia ya wanachama wa Vicoba Endelevu kutoka sehemu
mbalimbali nchini.
Benki
ya Posta Tanzania, imeingia mkataba na Vicoba Endelevu, wa kuwapatia mikopo
midogomidogo wananchama hao chini ya udhamini wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji
Wananchi Kiuchumi, NEEC, ili kukuza mitaji na kuendeleza shughuli zao za
kiuchumi.
Wana VICOBA Endelevu wakiingia kwenye bustani hiyo kwa maandamano.
No comments:
Post a Comment