MGOMBEA URAIS WA UKAWA ALIVYOTAMBULISHWA JIJINI MBEYA JANA
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha
Demokrasia na Maendeleo, Mh. Edward Lowassa akiwapumbia maelfu ya wafuasi
na wapenzi wa vyama vinavyounda UKAWA waliofurika kwa wingi kwenye
Uwanja wa Rwanda Nzovwe, Jijini Mbeya jana Agosti 14, 2014. Mh.
Lowassa na Mgombea mwenza wake Dkt. Juma Haji Duni, walikuwa jijini humo
kwa ajili ya zoezi la kutafuta wadhamini wa Tume na kutambulishwa kwa
wananchi.
Mbunge
wa Jimbo la Mbeya Mjini, Mh. Joseph Mbilinyi "Sugu" akimueleza jambo
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama
cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Edward Lowassa, wakati akiwahutubia wafuasi
na wapenzi wa vyama vinavyounda UKAWA waliofurika kwa wingi kwenye
Uwanja wa Rwanda Nzovwe, Jijini Mbeya jana Agosti 14, 2014.
Mgombea
Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia
Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Dkt. Juma Haji Duni akiwahutubia
maelfu ya wafuasi na wapenzi wa vyama
vinavyounda UKAWA waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Rwanda Nzovwe,
Jijini Mbeya jana Agosti 14, 2014.
Mwenyekiti
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Freeman Mbowe akipunga mkono
pamoja na wafuasi na wapenzi wa vyama vinavyounda UKAWA waliofurika kwa
wingi kwenye Uwanja wa Rwanda Nzovwe, Jijini Mbeya jana Agosti 14,
2014.
KUONA PICHA ZAIDI
No comments:
Post a Comment