JESHI LA MAGEREZA LAIBUKA MSHINDI WA JUMLA MAONESHO YA WAKULIMA NANE NANE KIKANDA TAASISI ZA MAJESHI YA ULINZI NA USALAMA
Mkuu
wa Magereza Mkoani Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza,
Antonino Kilumbi akiwa ameshika vikombe vya ushindi katika Maonesho ya
Nane Nane Kanda ya Kati kwa Mwaka 2015. Wengine ni Maafisa Washiriki wa
Jeshi la Magereza wa Maonesho ya Wakulima ya Nane Nane Kanda ya Kati,
Dodoma.
…………………………………………………………………
Jeshi la Magereza nchini limeibuka
Mshindi wa kwanza kwa upande wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama katika
Maonesho ya Nane Nane yaliyofanyika katika Kanda ya Kasikazini(Mikoa ya
Arusha, Kilimanjaro na Manyara), Kanda ya Magharibi(Mikoa ya Morogoro,
Pwani, Tanga na Dar es Salaam) pamoja na Kanda ya Magharibi(Mikoa ya
Tabora, Kigoma na Shinyanga) ambapo Jeshi la Magereza limeibuka kidedea
katika upande wa Uzalishaji Taasisi za Serikali pamoja na Taasisi za
Serikali upande wa Teknolojia na Maonesho Vyombo vya Ulinzi na Usalama.
Jeshi la Magereza ni Miongoni mwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama vilivyopo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi likiwa na jukumu lake la kuwahifadhi na kuwarekebisha Wafungwa wa aina mbalimbali wawapo Magerezani ili pindi wamalizapo vifungo vyao waweze kuwa raia wema katika jamii. Pia hushiriki kikamilifu katika Maonesho ya Nane Nane Kitaifa na Kikanda kwa lengo la kutoa elimu kwa umma kupitia shughuli zake mbalimbali za uzalishaji katika Sekta za Kilimo na Mifugo.
No comments:
Post a Comment