CHAMA CHA MAPINDUZI CCM ZANZIBAR CHATOA TAMKO JUU YA KUJITOA KWENYE CHAMA WAZIRI MKUU MSTAAFU EDWARD LOWASA.
Katibu
wa CCM Mkoa Mjini Mohammed Omar Nyawenga akitoa taarifa ya Chama hicho
kwa Waandishi wa Habari kuhusu kujitoa ndani ya Chama Waziri Mkuu wa
zamani Edward Lowassa katika mkutano uliofanyika Afisi Kuu ya CCM
Kisiwandui.
Baadhi ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakifuatilia mkutano huo uliofanyika Afisi Kuu ya CCM aKisiwandui Mjini Zanzibar.
Mwenyekiti
wa CCM Mkoa Mjini Borafia Silima akitoa ufafanuzi katika mkutano
uliohudhuriwa na wajumbe wa ngazi mbali mbali za Chama na waandishi wa
Habari Afisi kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.
Na Mwashungi Tahir/Maryam Kidiko -Maelezo Zanzibar
Chama
cha Mapinduzi (CCM) kimesema ni Chama kikubwa chenye wafuasi na
wanachama wengi pamoja na Viongozi wenye hekima, busara, mapenzi na
uadilifu mkubwa.
Hayo
yameelezwa na Katibu wa CCM Mkoa Mjini Mohammed Omar Nyawenga wakati
alipokuwa akitoa taarifa kwa Waandishi wa Habari kuhusu kujitoa Chama
cha Mapinduzi Waziri Mkuu wa zamani Edward Ngoyai Lowassa na kujiunga na
Chama cha upinzani huko Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui
Amesema
CCM ni Chama kinacho aminiwa na kukubalika na Wananchi wengi wa
Tanzania hivyo kujitoa kwa mwanachama mmoja ama kikundi cha wanachama
haiwezi kukiathiri chama hicho.
Nyawenga
ameongeza kuwa wingi wa wanachama wa chama hicho haujaletwa na utajiri
wa vingozi wake bali umetokana na uimara wa Siasa, Sera na itikadi
yake.
Alisema
CCM haina hasara kumpoteza mwanacham mmoja anaetaka kubadili sera na
itikadi ya Chama kwa maslahi yake binafsi na marafiki zake hata kama
utajiri wake ni mkubwa wa kupindukia.
Ameongeza
kuwa uwamuzi wa Lowassa kujiondowa ndani ya Chama hicho sijambo la
kukishituwa chama, viongozi, pamoja na wanachama wake na hakiwezi
kudhoofika wala kutetereka.
Alisema
hii sio mara ya kwanzi kwa Chama cha Mapinduzi kuondokewa na kiongozi
mwandamizi na kujiunga na vyama vya upinzani na bado kinaendelea
kuimarika.
“Mwaka
1989, CCM iliwafukuza uanachama viongozi waandamizi 11 akiwemo Waziri
Kiongozi mstaafu wa Zanzibar Seif Sharif Hamad, akafuatia Agostino
Lyatonga Mrema na mwaka jana CCM ilimfukuza uanachama aliyekua
Mwakilishi wa Kiembesamaki Mansour Yussf,” alikumbusha Katibu wa Chama
Mkoa.
Nyawenga
aliweka wazi kuwa umaarufu alionao Lowassa inawezekana umejengwa
kutokana na CCM lakini haiwezekani umaarufu wa Chama hicho umejengwa
kutokana na yeye.
Alisema
wanachama wa Zanzibar waliokuwa wakimuunga mkono Lowassa katika azma
ya kuomba kuteuliwa na CCM kuwa mgombea wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania walifanya hivyo kwa sababu ya siasa, sera na ilani
ya Chama na sasa baada ya kuhama wameamua kujitenga na hawako pamoja
naye.
Mwenyekiti
wa Mkoa wa Mjini Magharib Borafia Silima amesema kwamba Tanzania
inaheshimika kuwa ni nchi yeye amani, na mshikamano na Chama cha
Mapinduzi kinafuata utaratibu wa katiba iliyowekwa.
No comments:
Post a Comment