RAIS KIKWETE: PSPF ENDELEENI KUTOA ELIMU YA MPANGO WA UCHANGIAJI WA HIARI
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi
Mkuu wa PSPF Bw. Adam Mayingu alipotembelea banda la PSPF katika sherehe za
siku ya Magereza zilizofanyika Ukonga jijini Dar es Salaam Mwishoni mwa wiki
iliyopita.
·
Wengi
wajiuga na Mpango huo.
RAIS wa Jamhuri ya
muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameushauri Mfuko wa
Pensheni wa PSPF kuendelea kutoa elimu ya Mpango wa uchangiaji wa hiari kwa
watanzania.
Mheshimiwa Rais
alisema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita katika siku ya Magereza alipotembelea
banda la PSPF katika maonesho maalum yaliyoandaliwa kwa ajili ya siku hiyo.
Akiwa katika banda la
PSPF Mheshimiwa Kikwete alikaribishwa na Mkurugenzi Mkuu wa PSPF Bw. Adam
Mayingu ambaye pamoja na mambo mengine alimjulisha juu ya juhudi za PSPF za
kuhakikisha kila mtanzania anakuwa katika hifadhi ya jamii kwa kupitia Mpango
wa Uchangiaji wa Hiari wa PSPF.
Katika mpango huo
mtanzania yeyote aliye katika sekta rasmi na isiyo rasmi anaweza kuwa
mwanachama ili mradi awe amefikisha umri wa miaka 18, kiwango cha chini cha kuchangia
ni shilingi 10,000 kwa mwezi. Mpango huu ni mkombozi kwa watanzania.
Rais kikwete
alifurahishwa na mpango huyo na alimweleza Mkurungezi Mkuu wa PSPF, “Safi sana
endeleeni na Mpango huu”.
No comments:
Post a Comment