Header Ads

LEMA KUPEPERUSHA BENDERA YA CHADEMA NA JOYCE MUKYA

SAM_4216Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema akizungumza katika uchaguzi wa kumpata Mbunge pamoja na Mbunge viti maalum kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo(CHADEMA)jijini Arusha ambapo aliibuka kidedea kwa kura 255 sawa na asilimia 93.06% (Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
SAM_4210Mbunge viti maalum kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Joyce John Mukya alipata kura 39 sawa na asilimia 73.6% katika kinyang'anyiro hicho hivyo kumfanya kuwa Mbunge wa viti maalum,aliwataka wajumbe wa mkutano huo kuvunja makundi ili kuhakikisha chama kinashinda katika uchaguzi wa Urais,Ubunge na udiwani
SAM_4212 Mgombea kupitia chama cha Demokrasia na maendelao (CHADEMA)Noel Olevaroya akizungumza mara baada ya kutangazwa kushika nafasi ya pili  kwa kupata kura 13 sawa na asilimia 4.74% katika kinyang"anyiro hicho ambapo aliwashukuru wajumbe wa mkutano huo na kuhaidi kumpa Mbunge Lema shilingi laki tano kwaajili ya kampeni ya kuhakikisha  chama hicho kinapata ushindi wa kishindo
SAM_4147Wagombea ubunge viti maalum Mkoa wa Arusha wakisubiria kuingia kujinadi kwa wajumbe wa mkutano.

No comments:

Powered by Blogger.