KONGAMANO LA TAMASHA LA 20 LA UTAMADUNI WA MZANZIBAR LAFANYIKA JANA
Mshereheshaji katika Kongamano la Tamasha la 20 la
Utamaduni wa Mzanzibar Otman Mohd (Makombora ), akitoa maelezo mafupi ya
kongamano litakavyokuwa katika Ukumbi wa Suza mjini Zanzibar.
Baadhi ya Washiriki wa Kongamano la Tamasha la 20 la Utamaduni
wa Mzanzibar wakisikiliza kwa makini mada inayowasilishwa katika Ukumbi
wa Suza mjini Zanzibar.
Katibu
mtendaji wa Baraza la Kiswahili Zanzibar Bimwanahija Ali Juma ambae ni
mgeni rasmi akitoa hotuba ya ufunguzi wa Tamasha la 20 la Mzanzibari
katika Ukumbi wa Suza mjini Zanzibar.
Mtoa mada Bimwanahamisi Hamadi akiwasilisha mada ya Athari za
Utalii katika kuendeleza Utamaduni katika Tamasha la 20 la Mzanzibari
katika Ukumbi wa Suza mjini Zanzibar.
Mmoja kati ya washiriki wa Tamasha la 20 la Mzanzibari Abdalla
Alawi akichangia mada iliowasilishwa katika Tamasha hilo katika Ukumbi
wa Suza mjini Zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.
No comments:
Post a Comment