Header Ads

TUME YA HAKI ZA BINADAMU, UNESCO WATAKA JAMII KUTAMBUA WATU WENYE ALBINISM


XXKamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Dkt. Kevin Lothal Mandopi akielezea namna ya tume hiyo ilivyo mstari wa mbele kuelimisha Umma dhidi ya vitendo na ukatili kwa watu wenye Ualbinism nchini kwa wadau na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam mapema leo Juni 13.2015.

Na Andrew Chale, modewjiblog
Tume ya Haki za binadamu na Utawala bora nchini, leo Juni 13,2015, imeungana na watanzania wote kuadhimisha siku ya Kimataifa ya uelimishaji umma kuhusu Ualbino na haki za watu wenye Ualbino ambapo imeitaka jamii kutambua haki na wajibu wa kuwalinda na kuwathamini.

Akisoma taarifa maalum kwa wadau mblimbali na waandishi wa habari waliojitokeza jijini Dar Es Salaam, Kamishna wa tume hiyo, Dkt. Kevin Lothal Mandopi alieleza kuwa jamii inayo wajibu wa kuwathamini watu hao wenye albinism kwani nao ni kama binadamu wengine na wana haki sawa.

Kamishna Mandopi katika taarifa hiyo alibainisha kuwa, mpango wa elimu kwa umma umelenga kubadilisha fikra, mtazamo na imani potofu juu ya watu wenye ualibinism. “Ni dhahiri kuwa iwapo jamii itaelewa dhana nzima ya Ualbinism na kubadili fikra na dhana potofu dhidi ya watu hawa, kuna uwezekani mkubwa wa kukomesha kabisa matendo maouvu dhidi ya ndugu zetu wenye Ualbinism” alieleza Kimishna Mandopi.
UNS
Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues akizungumza kwa msisitizo juu ya jamii ya watanzania kuchukua hatua ya kuwalinda watu wenye Ualbinism nchini wakati wa tukio maalum la maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Uelimishaji Umma kuhusu Ualbino, iliyoandaliwa na tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini. 

kushoto kwake ni Wakili wa Serikali na Mratibu wa masuala ya Albinism nchini, Bi Beatrice Mpangala. Kwa upande wake Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi. Zulmira Rodrigues alisisitiza jamii nchini kuongeza upendo pamoja na kuachana na imani potofu inayosababisha kukithiri kwa vitendo hivyo hapa nchini.

No comments:

Powered by Blogger.