KATIBU MKUU WA CHADEMA DKT. WILLIBROD SLAA ZIARANI BARANI ULAYA

Katibu
Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa
ameondoka nchini Jumamosi Juni 06, 2015 kuelekea Bara la Ulaya ambako
atakuwa na ziara ya kikazi ya siku nane.
Akiwa
ziarani Dk Slaa anatarajiwa kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi
mbali mbali wa nchi za Jumuiya ya Ulaya (EU) ambapo pia atakutana na
jopo la wataalamu wa masula ya uchumi kwa lengo la kubadilishana uzoefu
katika kupata mifumo sahihi na kujenga taasisi za kusaidia uwajibikaji
na kusukuma maendeleo ya watu katika nchi za Afrika hususan zile zenye
rasilimali nyingi kama Tanzania ili kuziepusha na kile ambacho
kimezikumba nchi nyingi duniani yaani ‘laana ya raslimali’ (resource
curse).
Aidha,
akiwa na viongozi wa nchi za Ulaya, Dk Slaa atajadiliana nao kuhusu
hali ya Demokrasia, utawala bora na hali ya haki za binadamu nchini hasa
kwa kipindi hiki ambapo Watanzania wanaelekea kwenye uchaguzi mkuu
mwezi Oktoba. Katika ziara hiyo, viongozi hao wa Ulaya watapata fursa ya kujadiliana na Dk. Slaa hali ya siasa kwa Ukanda wa Afrika Mashariki.
Katika
ziara hiyo Katibu Mkuu Dk. Slaa ameambatana na Mkurugenzi wa Bunge na
Halmashauri, John Mrema na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano,
Tumaini Makene.
Itakumbukwa
kuwa Katibu Mkuu Dk. Slaa amekwensa ziarani barani Ulaya akiwa ametoka
kufanya ziara ya kikazi katika maeneo mbalimbali ya mikoa ya Kagera,
Mbeya, Rukwa na Katavi akikagua zoezi la uandikishaji wapiga kura kwenye
Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Kwa mfumo wa BVR huku pia
akiwahamasisha Watanzania wote wenye sifa za kupiga kura kuhakikisha
wamejiandikisha.
Alitumia
pia ziara hiyo kukagua maandalizi ya chama katika maeneo mbalimbali kwa
kushirikiana na vyama washirika wenza katika UKAWA kushinda uchaguzi
mkuu wa mwaka huu.
Dk. Slaa atarejea nchini tarehe 15.06.2015.
No comments:
Post a Comment