January Makamba: Sigombea Kupambambana na Mtu bali Kupambana na Matatizo ya watanzania.
Mh
Naibu wa waziri wa Sayansi na Teknolojia na Mtangaza nia kugombea nafasi
ya Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, January Makamba
anaendelea na Ziara yake ya Kusaka wadhamini katika mikoa mbalimbali ya
Tanzania.
Mgombea
huyo leo alikua Singinda kuomba udhamini na kapata udhamini wa kutosha
kwa wanachama wa CCM singinda, Mbali na hilo Mh January alizaliwa katika
mkoa huo wakati baba yake mzee Yusuph Makamba akiwa mkoa huo kikazi.
Wanasinginda
wamemsikiliza kwa makini Mh January na kuamini kuwa ni kija ambaye
ataleta mabadiliko kutokana na majawabu yake juu ya kero mbalimbali
ambazo zinawakabili watanzania walio wengi.
January
Makamba aliwambia wanasinginda kuwa wananchi wanaitaji mabadiliko na
wasipoyapata ndani ya CCM watayafuata nje ya CCM, kauli iliyosemwa na
Baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere, Makamba amewaeleza kuwa ili
mabadiliko hayo yatokee ni lazima wachague kiongozi wa aina yake ambaye
akipanda jukwaani hana mzigo wowote wala hatotumia muda mwingi
kujielezea lakini pia anaomba nafasi hiyo sio kwa ajili ya kumkomoa wala
kupambana na mtu yeyote bali ameomba nafasi hiyo kupambana na matatizo
pamoja na changamoto za watanzania.
No comments:
Post a Comment