WAKUU WA TAASISI ZA TAKWIMU WA NCHI ZA AFRIKA WAKUTANA JIJINI DAR
Mtendaji
Mkuu wa Taasisi ya Takwimu ya Bara la Afrika Bw. Joseph ILboudo
akizungumza na watalaam na wakuu wa Ofisi za Takwimu Kongamano la
Kimataifa kuhusu Uongozi na utawala lililowahusisha wataalam na Wakuu wa
Taasisi za Takwimu wa nchi za Afrika zinazozungumza lugha ya
Kiingereza na Kifaransa leo jijini Dar es salaam.
Bw.
Andry Andriantseheno kutoka UNECA akiongoza kongamano hilo la siku 2 la
watalaam na wakuu wa Ofisi za Takwimu wa nchi za Afrika linalojadili
masuala ya Uongozi na utawala na leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni
Dkt. Albina Chuwa, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu kutoka
Tanzania wenyeji wa mkutano huo.
Baadhi
ya watalaam na wakuu wa Ofisi za Takwimu kutoka katika nchi mbalimbali
za Bara la Afrika wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa kongamano la
Kimataifa kuhusu Uongozi na utawala linaloendelea jijini Dar es salaam.
Aliyekuwa
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Takwimu Barani Afrika (AFRISTAT) pia
mtaalam wa Takwimu kutoka nchini Cameroon Bw. Martin BALEPA akiwasilisha
mada kuhusu namna nchi za Bara la Afrika zinavyoweza kukabiliana na
changamoto mbalimbali kwa kutumia takwimu sahihi.

No comments:
Post a Comment