Tamko la Mhe. Nyalandu kuhusu shutuma za Mbunge Mhe. Nassari

“Nimesikitishwa sana na kauli ya
Mhe. Joshua Nassari ambayo ameongea kwa kudhalilisha utendaji wangu serikalini.
Naomba Mh. Nassari afahamu kuwa
kunikashifu pasipo kueleza
masuala ya kisera au ya kiutendaji ni kupungukiwa na busara ya kawaida kwa kiongozi aliyepaswa
kuwawakilisha wapiga kura wake kwa hoja.
Itakumbukwa kuwa hivi karibuni Mhe.
Nassari aliniita Jimboni kwake Arumeru Mashariki
akiniomba nitatue tatizo lililohusu wananchi wa jimboni
kwake waliokuwa wanahitaji matibabu katika
hospitali ambayo ilikuwa
sharti upitie ndani ya hifadhi
ili ufike kutibiwa.
Nilikwenda kuwaona wagonjwa na kuitembelea hospitali
hiyo na kulitatua tatizo hilo siku hiyo
hiyo. Kwangu kama Waziri, halikuwa suala la kufanyia siasa
afya za Watanzania, pamoja na yeye kuwa Mbunge wa upinzani.
Nilimheshimu
na kukubali wito wake kwa niaba ya wananchi.
Nimewatembelea na kuwatia moyo
maaskari wetu nchi nzima na kuwapelekea vitendea kazi. Nimefurahi pamoja nao na kulia pamoja nao. Nimeenda kuwafariji familia
za wapiganaji wetu waliopoteza maisha
kwa kuuawa wakilinda raslimali za Taifa, watu ambao Mhe. Nassari anawabeza.
Tumepambana na
ujangili na tunaendelea kuushinda. Tumeleta magari, silaha, ndege, helicopters, na raslimali nyingi ili
kulinda raslimali za Taifa. Busara
haisomewi ila ni kumshukuru Mungu
akusaidie kujua matumizi ya
ulimi. Nimesikitishwa sana na kauli za
uongo na kuzusha za Mhe. Nassari. Imeandikwa, usimsingizie jirani yako uongo.”
Mh. Lazaro Nyalandu.
No comments:
Post a Comment