SHIGONGO AZINDUA VITABU VYAKE VITATU VIPYA KATIKA OFISI ZA GLOBAL
MHAMASISHAJI
na mjasiriamali wa kimataifa, Eric James Shigongo, amewaasa Watanzania
kutokata tamaa katika kufuatilia ndoto zao huku wakiamini kuwa wao ni
watu muhimu katika maisha yao na ya jamii.
Akizungumza
na vyombo vya habari mapema leo ndani ya ofisi za Global Publishers
zilizoko Mwenge-Bamaga jijini Dar katika uzunduzi maalumu wa vitabu
vyake vitatu, Shigongo aliwataka Watanzania kuwa na tabia ya kusoma
vitabu ili kupata maarifa mengi ya juu ya mafanikio maishani.
“Kila
mmoja ana ndoto za kufikia malengo yake ikiwa ni pamoja na kuondoka
mahali alipo. Wengi hushindwa kupiga hatua za mafanikio maishani kwa
sababu nyingi yakiwemo mazingira waliyokulia wakiaminishwa kuwa hawawezi
kufanya chochote maishani, jambo ambalo si la kweli kwani kila mmoja
anaweza kufikia ndoto zake akiamua tu kubadili fikra na namna ya kutenda
mambo maishani,” alisema Shigongo.
Vitabu
vilivyozinduliwa ni ‘Sheria 10 Zilizothibitishwa – Jinsi ya Kutoka
Kwenye Umaskini Hadi Mafanikio’, cha pili ni ’10 Proven Secrets – How to
Move From Poverty to Success’ na cha tatu ni ’26 Secrets – How to
Defeat Your Enemies and Make Millions of Dollars’.
Uzinduzi
wa vitabu hivyo ni kuashiria kwake kuingia rasmi mitaani na kusambazwa
kwenye kona mbalimbali ndani na nje ya nchi ambapo vinatarajiwa
kubadilisha maisha ya maelfu ya wasomaji watakaofanikiwa kupata siri za
mafanikio.
No comments:
Post a Comment