RAIS KIKWETE AWAAPISHA KATIBU MKUU, NAIBU KATIBU MKUU WA MAMBO YA NJE NA BALOZI WA TANZANIA SAUDIA
![]() |
| Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha Balozi Liberata Mulamula kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Balozi Mulamula anakuwa Katibu Mkuu wa kwanza mwanamke kuongoza Wizara hiyo na kabla ya uteuzi huo alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani. Hafla hiyo fupi ya uapisho imefanyika Ikulu tarehe 27 Mei, 2015. |
![]() |
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete
akishuhudia Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Balozi Mulamula akisaini Hati ya Kiapo mara baada ya
kumwapisha.
|
![]() |
| Mhe. Rais Kikwete akimkabidhi Balozi Mulamula Vitendea Kazi mara baada ya kumwapisha. |
![]() |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha Balozi Hassan Simba Yahya kuwa
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa. Kabla ya uteuzi huo Balozi Yahya alikuwa Mkurugenzi wa Idara
ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa. Hafla hiyo fupi ya uapisho imefanyika Ikulu tarehe 27 Mei,
2015.
|
![]() |
Mhe.
Rais Kikwete akishuhudia Naibu Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Yahya akisaini Hati ya Kiapo
mara baada ya kumwapisha.
|
![]() |
| Mhe. Rais Kikwete akimpongeza Balozi Yahya mara baada ya kumwapisha kuwa Naibu Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. |
![]() |
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete
akimwapisha, Mhe. Hemed Iddi Mgaza kuwa Balozi wa Tanzania nchini Saudi
Arabia. Kabla ya uteuzi huo Balozi Mgaza alikuwa Afisa Mambo ya Nje
Mkuu na Mkuu wa Utawala katika Ubalozi wa Tanzania, Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo (DRC). Hafla hiyo fupi ya uapisho imefanyika Ikulu
tarehe 27 Mei, 2015.
|







No comments:
Post a Comment