Mkuu
wa Mkoa wa Singida- Mh. Dk. Perseko Vincent Kone (kati) akikata utepe
kuzindua rasmi tawi la Singida, kushoto ni Meneja wa NMB Kanda ya Kati
Bw. Ole Loibanguti na Meneja wa NMB tawi la Singida- Bi. Christine
Mwangoma.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida- Mh. Dk. Perseko Vincent Kone akipata maelezo
kuhusu huduma na bidhaa zinano tolewa katika tawi hilo kutoka kwa
Meneja wa NMB tawi la Singida - Bi. Christine Mwangoma.
Benki ya NMB imefungua rasmi tawi lake jipya la Singida. Tawi hilo
litakuwa na huduma zote za kibenki kama yalivyo matawi mengine ya NMB
nchini…

nchini kote. Tawi hili limefunguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mh. Dk.
Perseko Vincent Kone.
Kufunguliwa kwa tawi la Singida sasa kutaharakisha maendeleo ya
wakazi wa Mkoa wa Singida na pia kurahisisha biashara kati ya wananchi
wa mji huo na wa maeneo ya jirani. Hii ni kwa sababu NMB sasa
inawezesha wateja wake kuuza, kununua, kutuma na kupokea fedha za kigeni
popote ulimwenguni tena kwa gharama nafuu. Kwa hili biashara itaimarika
na ubadilishaji wa fedha za kigeni utakuwa rahisi kupita hapo awali,
hasa tukifahamu kua Singida ni sehemu ya biashara na wafanyabiashara
mbali mbali hutembelea mkoa huo.
Kwa kutambua pia nia ya kuendelea kuchangia huduma mbali mbali za
kijamii, benki ya NMB imetoa shilingi Milioni 25 kwa ajili ya hospitali
na shule kama shukrani za Benki kwa wananchi wa Singida kwa kuendelea
kwao kuunga mkono maendeleo ya benki.
NMB ndiyo benki inayoongoza
nchini kwa kuwa na matawi mengi kwani ina matawi zaidi ya 160, ATM zaidi
ya 600 nchi nzima pamoja na idadi kubwa ya wateja.
Kwa mawasiliano zaidi, wasiliana na: NMB Singida;
S.L.P 1040
Singida
Simu: 026 2540328
: 026 2540145
No comments:
Post a Comment