MASHARTI MAGUMU YAPIGILIA MSUMARI WAGOMBEA CCM, NGOMA YAWA NGUMU ZAIDI.

* Mbwembwe,sherehe marufuku
*Idadi ya wadhamini, mikoa sasa yaongezwa
*Wajumbe NEC, marufuku kudhamini wagombea
*Idadi ya wadhamini, mikoa sasa yaongezwa
*Wajumbe NEC, marufuku kudhamini wagombea
Chama
cha Mapinduzi(CCM), kimetangaza rasmi ratiba ya kuchukua na kurejesha
fomu kwa ajili ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ikiwemo ya
urais, huku kikitoa masharti magumu kwa wanaotaka kuwania urais kupitia
chama hicho.
Chama
hicho kimetoa msimamo wake kuwa wagombea wanatakia kuheshimu kanuni na
misingi ya chama hicho na ni marufuku kwa wagombea kufanya mbwembwe,
madoido na kukodi watu kwa ajili ya kukushangilia wakati wa kuchukua
fomu au kurudisha ni marufuku.
Akitangaza
uamuzi wa wajumbe wa Halmashauri Kuu(NEC) ya chama hicho, leo mjini
Dodoma,Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amesema fomu ya
kugombea urais itaanza kutolewa Juni 3 mwaka huu na kuzidurisha Julai 2
mwaka huu saa 10 jioni.
Amesema
kuanzia Juni 3 wanaruhusiwa kuanza kuchukua fomu na kuzirudisha Julai 2
mwaka huu. Wakishachukua fomu watafanya kazi ya kutafuta wadhamini
mikoani. Amesema
mwaka huu idadi ya wadhamini imeongezeka kutoka wadhamini 250 hadi
wadhamini 450 huku idadi ya mikoa nayo ikiongezeka kutoka 10 hadi 15.
Nape
amesema kuongeza kwa wadhamini hao ni kutokana na idadi ya wanachama
wao kuongezeka na wakati huo huo mikoa nayo imeongezeka.Hivyo lazima
wagombea waende kwenye mikoa hiyo ambapo mikoa 12 kwa Tanzania Bara na
mikoa mitatu Zanzibar na moja ya mkoa uwe Pemba au Unguja.
Amesema
moja ya sharti ni kuhakikisha wadhamini wa mgombea mmoja wa ngazi ya
urais hawatakiwi kuwa wadhamini wa mgombe mwingine .Hivyo kila mdhamini
mmoja anatakiwa kumdhamini mgombea mmoja na si zaidi.
“Tumekubaliana
kwenye NEC mwanachama mmoja anatakiwa kumdhaminni mgombea mmoja
tu.Haitaruhusiwa mwachama mmoja kuwadhamini wagombea wawili.
Pia
amesema wakati wa kuchukua fomu na kurejesha ni marufuku mgombea
kufanya mbwembwe za aina yoyote huku akifafanua ni muhimu wagomba kusoma
kanuni na kuzielewa mapema. Kwa
mujibu wa Nape ni kwamba vikao vya uchuchaji ni kwamba Kamati ya
Maadili na Usalama itachuja majina ya wagombea urais Julai 8 mwaka huu,
Kamati Kuu(CC) itachuja majina Julai 9 mwaka huu na Halmashauri Kuu nayo
itapitisha jina la mgombea Urais Zanzibar.
Wakati
kwa jina la mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jina
litapitishwa na wajumbe wa Mkutano Mkuu Julai 11 mwaka huu mjini hapa. Alisisitiza
wagombea urais wanatakiwa kuheshimu kanuni za chama hicho katika
mchakato mzima wa kuchukua fomu, kurudisha na hata wakati wa kutafuta
wadhamini na mwaka huu masharti yameongezeka kidogo likiwemo la idadi ya
wadhamini na wagombea kuhakikisha hawakiuki kanuni za maadili.
“Sharti
ambalo limetolewa na NEC ni kwamba marufuku wajumbe wa NEC na Kamati
kuu kuwadhamini wagombea urais kwani wao ndio watakaopitisha jina la
mgombe, hivyo hawatakiwi kua sehemu ya wadhamini.
.
Kuhusu
kuchukua fomu ya udiwani, ubunge na uwakilishi, Nape amesema fomu
zitaanza kutotolea Julai 15 mwaka huu na kurudishwa Julai 19 mwaka huu
wakati mikutano ya kempeni itaanza Julai 20 hadi Julai 31 mwaka huu.
Nape
alisema kura ya maoni itafanyika Agosti 1 mwaka huu wakati wabunge wa
viti maalumu nayo itakuwa Julai 15 mwaka huu na kurudisha fomu Julai 19
na kufafanua uchujaji wa majina utafanywa na Jumuiya ya Umoja wa
Wanawake(UWT), Taifa licha ya kwamba mchakato wake utapita Baraza la
Vijana.
Kwa
upande wa gharama za fomu kwa ajili ya kuwania nafasi mbalimbali za
uongozi kwenye chama hicho,Nape alisema fomu ya kugombea urais itakuwa
sh.milioni moja, wakati fomu ya kugombea ubunge ni sh.100,000 na fomu ya
udiwani sh.50,000.
No comments:
Post a Comment