LOWASSA KUANZA "SAFARI YA MATUMAINI" MCHANA WA LEO JIJINI ARUSHA

Gari
iliyombeba Mtangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha
Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward
Lowassa ikipita nje ya uwanja wa Sheih Amri Abeid, jijini Arusha mapema
leo asubuhi wakati akielekea kwenye Ofisi za CCM Mkoa. Mh. Lowassa
anatarajia kulihutubia taifa mchana wa leo kwenye uwanja wa michezo wa
Sheikh Amri Abeid, ikiwa ni sehmu ya kutangaza kwake nia yake ya kuwania
Urais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mtangaza
nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye
pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akisalimiana na
baadhi ya viongozi waliokuwepo kwenye ofisi ya CCM Mkoa wa Arusha.Kulia
ni Mkewe Mama Regina Lowassa.

Mtangaza
nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye
pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akisaini kitabu
cha wageni wakati alipotembelea ofisi ya CCM Mkoa wa Arusha. Kushoto ni
Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Ndg. Onesmo Ole Nangole.

Mwenyekiti
wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Ndg. Onesmo Ole Nangole akizungumza machache
mbele ya Mtangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi
(CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa
alieambatana na Mkewe, Mama Regina Lowassa pamoja na wanaCCM wengine.

Mh.
Edward Lowassa na Mkewe Mama Regina wakimsikiliza Mwenyekiti wa CCM wa
Mkoa wa Arusha, Ndg. Onesmo Ole Nangole (hayupo pichani).

No comments:
Post a Comment